Kikundi cha Filamu cha Kibaigwa Taijquan kimeachia
filamu yake ya nne inayoitwa Bakora chini ya usimamizi mkubwa wa kampuni ya
usambazaji ya Splash ambayo iko chini ya Step entertainment.
Akizungumza
na gazeti hili Mratibu wa kikundi hicho Yassin Kanyama alieleza kuwa utoaji wa
filamu hiyo ulikuwa ni mpango wa mwaka 2012
kwa ajili yakumaliza mkataba wa Splash waliosaini toka mwaka juzi ili
kuwa msambazji wao mkuu.
Alisema kwa
sasa filamu hiyo tayari imeingia mtaani kwa maana ya sokoni hivyo kwa wale
mashabiki wa filamu wanaweza kuipata kwenye maduka mbalimbali ya filamu.
“Tunawaomba
mashabiki wetu watuunge mkono kwa nunua filamu zetu kwa vile ndio ajira kubwa
tunayoitegemea vijana wengi kwa sasa, kwa kutuunga mkono kutatusaidia kutimiza
malengo yetu,”alisema.
Filamu ya
kwanza waliitoa mwaka 2010 ilikuwa ikijulikana kama ‘The killing of campsite’
ambayo ilichezwa ikiwa na mtindo wa kareti ambapo walikuwa wakifanya kazi na
Zena Video.
Filamu ya
pili waliitoa mwaka 2011 ilikuwa ikijulikana kama ‘Kahaba wa mapenzi’ ambapo
pia mtindo waliotumia ni ule wa kareti, wakati filamu yao ya tatu inaitwa Jitu
na ilifanikiwa kufanya vizuri na
kuwatangaza kwa kiasi kikubwa ambapo ilisambazwa na kampuni ya Splash.
Kanyama
alisema kwa jinsi ambavyo wanatoa filamu
moja ndipo wanapojifunza mambo mengi kwani kila moja hujifunza kulingana na
makosa wanayofanya hivyo pia huboresha yale mapungufu ili kutoa filamu ambazo
ni nzuri zaidi ya nyingine na kuweza kukubalika katika soko.
No comments:
Post a Comment