TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday 15 May 2012

Tukumbuke enzi za nyota wa Filipino 'Ina'



Kristine Hermosa 'Ina'
 Kristine Hermosa Orille amezaliwa  Septemba 9, 1983 mjini Quezon City, nchini Ufilipino. Ni mwigizaji maarufu kutoka nchi hiyo ambaye alishawahi kucheza tamthilia nyingi kama muhusika Mkuu akiwa na Jericho ama Angelo. Hermosa alizaliwa na matabaka mawili, mama yake ni mwispania na baba yake ni mfilipino.

Hermosa pia ana dada yake aitwae Kathleen, ambaye aliyekuwa na shauku ya kuwa nyota wa ‘’ABS-CBN’’. Ingawaje, dada yake Hermosa alifeli kumvutia mwamuzi katika uchaguzi wa kwanza wa wasanii, badala yake akachaguliwa mdogo wake mrembo mwenye sura ya kuvutia iliopelekea mwamuzi kumchagua, ni Kristine Hermosa, aliyechaguliwa kuwa msanii wa ‘’ABS-CBN’’.

Ilifikiriwa kuwa ni msanii mwingine tena mdogo mwenye urembo safi, aliyepatia umaarufu wake katika tamthlia ya "Pangako Sa 'Yo"  na The  Promise ambayo ndio iliomjengea umaarufu mkubwa sana kwa kuigiza kama mpenzi wake Angelo Buenavista (Jericho Rosales) ambaye baadae alikua mpenzi wake wa kweli wa katika maishani.

Miaka ya mwanzo kabla Kristine kuwa maarufu, aligiiza kama Baron Geisler katika tamhilia ya Nagbibinata. Baadae, alishriki katika mchezo mmoja wa kuigiza uliojulikana kwa jina la "Sa Sandaling Kailangan Mo Ako", mchezo huo ulikuwa ukionyesha kila siku za wiki, huku akiwa sambamba kabisa na mwigizaji mwenzake bwana Marvin Agustin.

No comments:

Post a Comment