TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 21 June 2012

Ben Paul amepanga kuimba na mama yake

Msanii wa Tanzania House of Talent (THT) Ben Paul amesema matarajio makubwa kimuziki kwa mwaka huu ni kumshirikisha mama yake mzazi ambaye ni msanii ambaye havumi lakini yumo katika makundi ya watu wanaojua kuimba.

Ben anasema kwamba mama yake ni mwanamuziki wa siku nyingi na amekuwa akiimba nyimbo za dini sema tu hajawahi kusikika wala kurekodi.

 “Nataka kuja tofauti, na nitamshirikisha mama yangu mzazi kwasababu ni mwimbaji mzuri wa muziki sema tu amekuwa akiimba zaidi nyimbo za dini, naamini atafanya vizuri,”anasema Ben Paul.

Toka ameingia THT tayari kwa mwaka huu amesharekodi nyimbo saba. Na ambazo zinavuma sana kwenye vituo mbalimbali vya redio na Runinga ni pamoja na Samboira, my number one na nyingine kibao. 

Anawaleza mashabiki wake kuwa kuna vitu vikali viko njiani hadi kufika mwishoni mwaka huu atakuwa ametoa nyimbo nyingi nzuri hivyo wakae mkao wa kula kungojea mashairi mazuri ya kuelimisha.

Msanii huyo ni miongoni mwa wasanii waliopata tuzo ya Kilimanjaro Award katika wimbo wake wa Samboira akiwa ni msanii bora anayeimba muziki wa taratibu kwa ladha inayowavutia wengi.

Mwanzoni wakati Ben anaanza muziki  alikuwa akifanya kazi na Studio moja iliyokuwa ikijulikana kama Muziki Laboratory ambapo ndipo alipotoa albam yake ya kwanza iliyokuwa ikijulikana kama ‘nikikupata’.
Wakati anaanza muziki huo Ben alikiri kutonufaika mwanzo kwasababu alitegemea kuwa angepata fedha za kutosha kwa ajili ya kuendelea na masomo yake ya Chuo Kikuu.

  Lakini kwa sasa anajivunia mafanikio baada ya kujiunga na Jumba la Sanaa (THT) kwa vile anaweza kupata shoo nyingi zinazomlipa. Kwa sasa ameweza kujiunga Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) ambapo anachukua masomo ya Benki.

No comments:

Post a Comment