TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday 25 July 2012

Dk.Kijazi awatoa wananchi hofu kuhusu hali ya hewa


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) Dk. Agnes Kijazi amesema upepo mkali unaovuma kwa sasa ni upepo wa kawaida ambao unakuwepo kila mwaka miezi hii na kuwahimiza wananchi kutokuwa na hofu dhidi ya hilo.

Akizungumza na blogu hii Ofisini kwake jijini Dar es Salaam Dk. Kijazi alisema mabadiliko yanayotokea hivi sasa ya hali ya hewa yasiwatishe watu.

Pia, alisema mafuriko yaliyotokea China hayawezi kufika Tanzania, kwa hivyo jamii isiwe na hofu. Vile vile alisema hiki sio kipindi cha mvua, msimu wake unaojulikana ni Octoba, Novemba, Decemba na kipindi cha mwezi Marchi, April na Mei.

Kipindi cha upepo ni Mwezi Juni, Julya na Agost. Pamoja na hayo alisema anatarajia kutoa taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa mapema mwezi Septemba mwaka huu hivyo wananchi waendelee kufuatilia ili kuchukua tahadhari.

No comments:

Post a Comment