TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Friday, 6 July 2012

Mawakili 286 wa kujitegemea wameapaishwa Dar

Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande
Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande amewaapisha mawakili 286 wa kujitegemea akiwemo Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe na kufanya idadi ya mawakili hao kufikia 2,602 nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha mawakili hao iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Jaji Chande alisema idadi ya mawakili wa kujitegemea hapa nchini ni ndogo ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki kama vile Kenya ambayo ina zaidi ya mawakili 10,000 wa kujitegema.

Aliwaeleza mawakili hao wasing’ang’ania  kukaa Dar es Salaam pekee kwa kuwa uwakilishi na huduma zao hazipo mjini tu bali zinahitajika hadi mikoani na hata katika maeneo ya vijijini.

No comments:

Post a Comment