Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa Watanzania saba
kucheza mpira wa miguu katika nchi za Kenya na Msumbiji.
TFF imetoa hati hizo kwa
wachezaji hao baada ya kuombewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF)
na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Msumbiji (FMF) ili waweze kucheza katika
klabu za nchi hizo.
Wachezaji waliokwenda Bandari ya
Kenya na klabu walizokuwa wakichezea nchini kwenye mabano ni David Naftali
(huru), Meshack Abel (huru), Mohamed Banka (huru) na Thomas Mourice (Mtibwa
Sugar).
Klabu ya CD Madchegde ya Msumbiji
imewachukua wachezaji Hassan Hassan Mustapha kutoka Mgambo Shooting ya Tanga,
na Abdallah Ally Abdallah na Thobias David Silas kutoka klabu ya daraja la kwanza
ya Transit Camp ya Dar es Salaam
Source:Full Shangwe blog
No comments:
Post a Comment