TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday 2 July 2012

Wafanyakazi wanne wa kigeni waliotekwa Kenya waachiwa huru

Na Mwandishi wetu

Wafanyakazi wanne wa kigeni waliotekwa katika kamp ya wakimbizi iliyo karibu na mpaka wa Somalia nchini Kenya wameachiwa huru na wako salama.

 Kamanda wa kijeshi wa Somalia alisema wafanyakazi hao wanne wako huru baada ya kufanyika kwa opehseni ya kuwaokoa usiku na mchana.

 Wageni kutoka Canada, Norway, Pakistan na Philippines, waliokuwa wakifanya kazi katika Baraza la wakimbizi la Norwegian walitekwa huku dereva wa Kenya akifariki dunia katika mashambulizi ya watekaji nyara wa kisomalia.

 "Wako salama mikononi mwetu,”Alisema Msemaji wa Jeshi la Kenya Cyrus Oguna alipokotiwa na AFP

Alisema "kwa msaada wa kikosi cha usalama cha Kenya na Somalia tulifanikiwa kuwatoa wafanyakazi hao baada ya mtekaji nyara mmoja kuuawa,”.

No comments:

Post a Comment