TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 9 August 2012

Tamko la Mkuu wa Sera ya Nje na Usalama wa Umoja wa Ulaya


Tamko la Mkuu wa Sera ya Nje na Usalama wa Umoja wa Ulaya, Catherine
Ashton, kwa niaba ya Umoja wa Ulaya katika Siku ya Kimataifa ya Watu
Wazawa Duniani tarehe 09 Agosti 2012

“Leo tunasherehekea Siku ya Kimataifa ya Watu Wazawa Duniani. Kwa niaba ya Umoja wa
Ulaya, naungana nao katika kusherehekea utajiri wa urithi wao na mchango wake kwa
ulimwengu.

Umoja wa Ulaya imekuwa inaunga mkono kuanzia mwanzo Tamko la Umoja wa Mataifa la
Mwaka 2007 juu ya Haki za Watu Wazawa. Tamko hili ni kifaa muhimu cha uhamasishaji juu
ya haki za binadamu, lakini utekelezaji wake ni ufunguo wa kufaidi hizo haki zenyewe. Umoja
wa Ulaya umerudia na kurudia wito wake wa kuzitaka nchi zote kuhakikisha hili
linatekelezwa.

Umoja wa Ulaya una historia ndefu wa kuhamasisha juu ya haki za binadamu za watu wazawa
katika nyanja zote za kazi yetu, katika kukutana na wawakilishi wa watu wazawa katika
majadiliano ya kisiasa na kutoa taarifa mbele ya Umoja wa Mataifa, kutoa msaada ya kifedha
kwa miradi ya asasi za kijamii.

Lakini tunaweza kufanya zaidi: na ndio maana, katika Mkakati Mpya wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, tumenuia kuangalia upya sera yetu na kuiboresha zaidi katika muktadha wa Tamko la Umoja wa Mataifa na katika maandalizi ya Mkutano wa Dunia wa Watu Wazawa utakaofanyika mwaka 2014.”

Nchi Mwanachama Kroashia*, Nchi zilizo katika mchakato wa kuwa wanachama Uturuki,
Jamhuri ya Masedonia zamani sehemu ya Yugoslavia*, Montenegro*, Iceland+ and Serbia*,
Nchi za Uthibiti na Mchakato wa Uhusiano na zinazoweza kuwa wanachama Albania na
Bosnia pamoja na Herzegovina, na nchi za EFTA yaani Liechtenstein na Norway, wanachama
wa Eneo la Uchumi la Ulaya, pamoja na Jamhuri ya Moldova, Armenia na Georgia, zinaunga
mkono tamko hili.

* Kroashia, Jamhuri ya Masedonia zamani sehemu ya Yugoslavia, Montenegro na Serbia
zinaendelea kuwa sehemu ya Uthibiti na Mchakato wa Uhusiano
+ Iceland inaendelea kuwa mwanachama wa EFTA na Eneo la Uchumi la Ulaya

Kutoka Brussels, Agusti 9, 2012

No comments:

Post a Comment