TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday 18 September 2012

Mafanikio ya mda mfupi yamefikiwa katika huduma ya afya

Lakini maboresho ya matokeo ya afya ya muda mrefu yahitaji kazi zaidi
 
  Mpango wa serikali wa kutoa kipaumbele katika usambazaji wa vyandarua kwa kaya umepata mafanikio makubwa. Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya kaya za Dar es Salaam zinamiliki angalau chandarua kimoja. Matumizi ya vyandarua ni hatua muhimu katika kuzuia mapambano dhidi ya malaria.
 
Hata hivyo wakati huo huo, zaidi ya nusu ya wakazi wa Dar es Salaam wametaarifu kuchemsha au kuwekea dawa maji yao kabla ya kunywa. Kwa vile idadi kubwa ya magonjwa yanayosababishwa na maji yanaweza kuzuiwa kwa kuwekea maji dawa ya klorini au kuyachemsha.Magonjwa hayo ni pamoja na kipindupindu na homa ya matumbo.
 
Hata hivyo uchache wa watu wanaokunywa maji safi ni changamoto kwa sekta ya afya kwa umma. Matokeo haya na mengineyo yameelezwa kwa kina kwenye muhtsari sera uitwao “Wakazi wa Dar wanasemaji kuhusu afya? Huduma za afya na utendaji katika Dar es Salaam” ambao umetolewa leo.

Muhtsari huu umejikita kwenye utafiti kuhusu utoaji wa huduma kwa umma uliofanywa na Uwazi iliyoko Twaweza kati ya Agosti na Septemba 2010. Jumla ya kaya 550 zilizochaguliwa kwa nasibu zilitembelewa na timu ya watafiti katika wilaya za Ilala, Temeke, na Kinondoni. Waliiulizwa kuhusu hali ya maisha ya wananchi na uzoefu wao wa huduma za umma.

Utafiti huu umeonyesha kuwa hali ya afya inaendelea kuwa changamoto kubwa kwa wakazi wa Dar es Salaam . Kaya moja katika kila kaya tatu imeripoti kuuguliwa na mtu miongoni mwa wanandugu wa kaya hiyo katika wiki iliyotangulia utafiti.
 
Cha kuogopesha ni kuwa , moja ya tatu ya kesi zilizoripotiwa ziliwahusu watoto, ambao mara nyingi wako katika hatari zaidi ya ugonjwa huo. Mafanikio yaliyopatikana katika hatua za msingi za kuzuia maradhi , kama vile usambazaji wa vyandarua vyenye dawa, ni hatua muhimu katika kuelekea kupambana na masuala ya afya ya umma. Hata hivyo kiwango cha watu wasiotumia maji safi kinaashiria tahadhari ya haraka yapaswa kuchukuliwa.

Utafiti zaidi kuhusu matokeo ya vituo vya afya pia umeonyesha baadhi matumaini, lakini kuna baadhi ya masuala muhimu ambayo bado yanahitaji kushughulikiwa.

  • Katika kaya ziliripoti kuwa zilikuwa na mgonjwa wiki kabla ya utafiti, asimilia 86 wamearifu kutafuta tiba katika kituo cha afya. Matumizi haya ya vituo vya afya ni hatua muhimu katika utambuzi sahihi wa ugonjwa na matibabu yake.
  • Kuna uhitaji mkubwa wa huduma ya vituo vya afya vya serikali, asilimia 60 ya washiriki wameaarifu kutumia vituo hivyo kwa ajili ya matibabu. Takwimu hizi zinaongezeka kwa kasi wakati kiwango cha kipato cha kaya kikihusishwa kwenye mchanganuo . Miongoni mwa kaya maskini zaidi, asilimia 82 hutumia vituo vya afya vya serikali.
  • Hata hivyo kuna tofauti katika kuridhika na huduma miongoni mwa wagonjwa kati ya hospitali binafsi na za umma . Asilimia 60 ya watumiaji wa vituo vya afya vya umma wamearifu kuridhika ukilinganisha na asimilimia 79% ya watumiaji wa hospitali binafsi.


Pamoja na mafanikio yaliyoonekana , Nyankomo Marwa, mtafiti mchambuzi wa Twaweza amesema " inafurahisha kuona mahudhurio ya juu ya wagonjwa kwenye vituo vya afya vya umma. Inaashiria kuwa wakazi wa Dar es Salaam wanapata pa kwenda kupata huduma wakiuugua. Hata hivyo hali iliyopo ya kutoridhika na hospitali hizi inaleta wasiwasi juu ya ubora wa huduma zinazotolewa. "

Muhtsari huu , umeonyesha kuwa kuna sababu ya kuwa na matumaini katika utoaji wa huduma ya afya jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, sera ya afya inapaswa kutoa kipaumbele katika mbinu zaidi za kuzuia magonjwa kama vile upatikanaji wa maji safi na salama. Ingawa upatikanaji wa huduma ya afya kwa umma unaonekana kuwajumuisha watu wa matabaka yote, kazi ya ziada inahitajika kufanywa ili kuhakikisha kwamba ubora wa huduma na matibabu katika hospitali hizi unaboreshwa, hasa katika suala la kupunguza kiwango kikubwa cha rushwa.

http://twaweza.org/go/wakazi-wa-dar-wanasemaji-kuhusu-afya

No comments:

Post a Comment