TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 21 February 2013

Daimond alalamika kuibiwa wimbo wakeMKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’ amewalalamikia watu ambao walimuibia simu yake na kuvujisha wimbo wake mpya ambao anatarajia kuuachia hivi karibuni.

Akielezea jinsi wimbo huo ulivovuja jijini Dar es Salaam , Diamond  alisema nyimbo zake huwa anazitunza katika simu yake ya mkononi na simu hiyo ilipoibiwa akasikia kwamba wimbo huo umeshanza kusikika mtaani.

“Wimbo unaitwa ‘Ukimuona’, ni kati ya nyimbo zangu ambazo zimesimama na zenye maneno Fulani ya kuwashika mashabiki, kiukweli mistari imesimama, naandaa video yake pamoja na kuvuja nitaitoa hivohivo maana ni bonge la ngoma,” alisema Diamond.
  
Alisema kazi hiyo ataiachia wiki ijayo anaomba mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani anaamini mistari ya kazi hiyo imesimama na inaujumbe katika jamii.

Diamond kwasasa anatamba na kibao chake cha ‘Kesho’ ambacho kimeliteka soko la muziki huo mbali na kuwa na vibao vingi ambavyo vinafanya vizuri.


No comments:

Post a Comment