TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 4 April 2013

Zawadi ya dola milioni 5 kumkamata Kony

Marekani imeahidi zawadi ya dola milioni tano kwa yeyote atakayetoa maelezo yatakayosaidia kukamatwa kwa kiongozi wa waasi wa Lords resistance Army nchini Uganda Joseph Kony.

Bwana Kony anadaiwa kuongoza maasi ya zaidi ya miongo miwili nchini Uganda na anatakiwa na mahakama ya kimataifa ya Uhalifu ICC kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita.

Kony na wapiganaji wake wako katika maficho yanayopakana na nchi jirani za Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ikiwemo Sudan, Jamuhuri ya kidemokrais ya Congo na Uganda.

Maafisa wa Marekani wanasema kuwa zawadi hiyo pia inatolewa kwa yeyote atakayetoa taarifa kuwahusu viongozi wengine wa waasi wa LRA Okot Odhiambo na Dominic Ongwen.
Kundi la LRA limewatesa watu na kuwadhalilisha watoto nchini Uganda, na kote katika eneo hilo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry alinukuliwa akisema kwenye jarida la Huffington Post siku ya Jumatano.

Bwana Kerry alisema kuwa Kony na viongozi wengine wa LRA , hawatapatikana kwa urahisi.
Kundi la LRA limetawanyika kwa makundi na waasi, walioko katika sehemu kubwa ya nchi kwenye maficho ambayo kwa kweli ni vigumu kuyapata, wakitawala eneo hilo kwa kutumia vitisho na kuwatia watu hofu.

Mapema, jeshi la Uganda katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, lilisitisha msako wao wa Kony na kurejea katika kambi zao za kijeshi.

Chanzo:Bbc Swahili

No comments:

Post a Comment