TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 27 May 2013

Flaviana azidi kung’ara Afrika, apata ‘dili’ la Truworths Afrika KusiniNa Mwandishi Wetu

MAMBO yanazidi kumnyookea mwanamitindo nyota wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata baada ya kuingia mkataba wa kutangaza nguo za  kampuni inayoongoza nchini Afika Kusini na Mashariki ya Kati, Truworths.  


Kampuni ya Truworths inaongoza kwa kuuza nguo za jumla na rejareja siyo Afrika Kusini ambapo kuna maduka  ya kuuza na kusambaza  zaidi ya 400 na kuwapa kibali cha kufanya biashara hiyo katika nchi  14 za Mashariki ya Kati (Middle East) na Afrika.  


Hatua ya Flaviana kupata nafasi hiyo imetokana na jina lake katika masuala ya maonyesho mbali mbali ya mitindo katika nchi hiyo, Uingereza na Marekani ambako ndiko anafanyia kazi kwa sasa.  


Flaviana ambaye pia ni Miss Universe wa mwaka 2007, ameweza kutangaza nchi nje ya mipaka yake kupitia masuala ya maonyesho ya mavazi na kwa sasa anaishi nchini Marekani kwa kufanya shughuli hiyo.  

Kuingia mkataba kwake katika kampuni hiyo kutampa nafasi kubwa ya kuinadi Tanzania kwani ni mwanamitindo pekee ambaye amepata nafasi hiyo kubwa nay a kujivunia.  


Akizungumzia nafasi hiyo, Flaviana alisema kuwa anashukuru Mungu kwa kupata mikataba mingi ya kufanya kazi za matangazo hasa kupitia mitindo kwa kampuni kubwa kama vile Diesel na  Edun.


 “Ni faraja kubwa kupata mikataba hii nah ii inatokana na juhudi zangu  za na mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai za kwa kuniongoza vyema, mpaka sasa nimeweza kushiriki katika matukio mengi ya kimataifa nje ya Tanzania na hasa katika nchi za Marekani na Uingereza,” alisema Flaviana.  


 Alisema kuwa kazi ya kuonyesha mitindo si kazi rahisi na ndiyo maana si kila msichana au mvulana anaweza kufanya kazi hiyo.
No comments:

Post a Comment