TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 30 May 2013

Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment yaandaa tamasha kuichangia familia ya Mangwea

R.I.P Mangwea

KAMPUNI ya QS Mhonda J Entertainment imeandaa tamasha la kuibua warembo bora linalofahamika kama QS Queen utamu extra  night likiwa na lengo la kuwapa mashabiki nafasi ya kuichangia familia ya marehemu Albert Mangwea aliyefariki hivi karibuni  nchini Afrika ya Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika ukumbi wa habari Maelezo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Fred Felix alisema tamasha hilo litafanyika Juni mosi katika ukumbi wa Dar Live Mbagala.

Felix alisema awali, kabla ya kifo cha msanii huyo tayari kampuni hiyo ilikuwa  imeshapanga kuwepo kwa tamasha hilo, hivyo baada ya kutokea kwa matatizo hayo, imeona isihairishe na badala yake waendelea na tamasha hilo kama ambavyo walipanga na fedha zitakazopatikana ziwe kama rambi rambi kwa familia ya msanii huyo.

“Tunatoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu Albert Mangwea ambaye tunatambua mchango wake katika tasnia ya muziki, baada ya kutafakari sana uongozi wa kampuni ukaona itakuwa ni jambo jema kuendelea na tamasha ili kuwapa mashabiki nafasi ya kuichangia familia yake,”alisema.
Alisema kutakuwa na kipindi maalum siku hiyo ambako kila ambaye atafika atapata nafasi ya kutoa rambi rambi zao na kuifikia familia ya marehemu kupitia kwa mwakilishi wa familia hiyo.

Amewaomba warembo mbalimbali wajitokeze siku hiyo na kutoa kiingilio cha sh. 10,000  ili waweze kujikatia tiketi ya ushiriki , ambapo miongoni mwa warembo watakaohudhuria  na kuonyesha vipaji vyao mbalimbali watachaguliwa walio bora zaidi kwa ajili ya kukaa ndani ya nyumba moja na warembo wengine ambao watatafutwa katika mikoa mingine.

Alisema baada ya tamasha hilo wataenda katika mikoa ya Mwanza, Mtwara, Mbeya, Singida, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha na mikoa mingine kwa lengo la kutafuta warembo wengine kisha kuwachanganya na wa Dar es Salaam watakaokaa jumba moja litakaloitwa QS Queens utamu extra house.

Felix alisema warembo hao watakaa  kwa miezi miwili huku wakiwa wanalipwa posho  na kupigiwa kura na wananchi kisha kutafuta mshindi wa jumla ambaye ataondoka na gari na ajira ya kudumu ambayo ni kuwa Balozi wa Kampuni hiyo. 

Baadhi ya wanamuziki wakali kama Ney wa Mitego, Madee, Juma Nature, Inspector Haroun, Mb Dog, Solid Ground Family, Hadija Kopa, Diamond na wengine kibao wataburudisha.

No comments:

Post a Comment