TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 30 May 2013

Shirikisho la muziki laomba mchango kwa watanzania kwa ajili ya kumsafirisha Mangwea



SHIRIKISHO la Muziki Tanzania (TMF) kwa kushirikiana na kamati ya kuratibu mazishi ya marehemu Albert Mangwea limewaomba watanzania kushiriki katika kuchangia fedha kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa msanii huyo kutoka Afrika Kusini kuja nyumbani Tanzania.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, viongozi wa TMF na kamati hiyo walisema  kwa  kuwa kuna gharama kubwa kama  vile kusafirisha mwili kutoka Afrika ya Kusini   na kuusafirisha mpaka Morogoro, usafiri, vyakula, viti, matangazo na malazi hivyo watanzania wachangie kufanikisha hayo.

Msemaji wa kamati  hiyo Adam Juma alisema wanatambua kwamba watanzania wanaukumbuka mchango wa marehemu jinsi alivyowahudumia kwa kuwaburudisha hivyo, wanaomba watanzania kujitokeza kwa wingi na kuchangia.

“Tunaomba tushirikiane sote kwa pamoja katika kipindi hiki kigumu ili kufanikisha yale tuliyopanga, ”alisema.
Alisema mchango unaweza kuwasilishwa kupitia M pesa ya kaka wa marehemu Keneth Mangwea 0754967738 au Tigo Pesa 0717553905.

Juma alisema wanampa pole mwanamuziki Mgaza Pembe M2P na kuomba maombi ya watanzania kumwombea na kuendelea kumchangia mwanamuziki huyo ambaye alikuwa Afrika Kusini na marehemu, ambaye mpaka sasa amelazwa katika hospitali ya St. Helen nchini Afrika Kusini.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho hilo Addo Mwasongwe amewaomba watanzania kutomtuhumu msanii marehemu Mangwea kwenye mitandano  na badala yake wasubiri kwanza uchunguzi kutoka katika hospitali ya St, Helen huku pia wakiendelea kumwombea.

Baadhi ya wasanii waliokuwepo katika mkutano huo na waandishi wa habari, walizungumzia jinsi walivyoguswa na msiba huyo na kusema hawatamsahau Albert Mangwea alivyokuwa mkarimu na mtu wa watu kwani alikuwa ni rafiki wa kila mtu.

Wasanii hao ni TID, Juma Mchopanga maarufu kama Jay Moe, Professa J, Noora, Mez B, mtayarishaji wa muziki P fun Majani na wengine.

Mwili wa Albet Mangwea utawasili Jumamosi jioni na kuhifadhiwa ambapo Jumapili kuanzia saa mbili asubuhi katika viwanja vya Posta au Leaders au Biafra utaagwa na wananchi na jioni kusafirishwa Morogoro Kihonda kwa ajili ya mazishi Juni 3.


No comments:

Post a Comment