TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Monday, 19 August 2013

Mkazi wa Kigoma ashinda gari la kwanza la tamasha la fiesta

Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya push Push Media Mobile Rugambo Rodney akimkabidhi namba ya gari/funguo mshindi wa kwanza wa gari aina ya Vitz iliyoendeshwa na kampuni hiyo kwa mashabikwa fiesta wa Kigoma. 


 Na Mwandishi wetu
MKAZI wa Kigoma, Abdallah Aly Ngagari (51) ameshinda gari aina ya Vitz iliyoendeshwa na kampuni ya Push Mobile Media ya kunogesha tamasha la Fiesta.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Kigoma, Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa tayari Ngagari amekabiziwa gari yake katika hafla fupi iliyofanyika huko huku Kigoma.
Rugambo alisema kuwa baada ya kukamilisha  bahati nasibu hiyo, kwa sasa nguvu zao wanazielekeza mkoani Tabora katika tamasha la Fiesta ambalo litafanyika Ijumaa.
Alisema kuwa watatoa pikipiki kwa wapenzi wa muziki wa Tabora ambapo ili kushinda, mashabiki wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kushinda pikipiki au fedha taslim shs 100,000.
“Tumepania kutoa zawadi katika mikoa yote ambayo Fiesta itafanyika, tumetenga zaidi ya sh milioni 80 ili kufanikisha zoezi hili ambapo magari aina ya vitz yapo nane kwa ajili ya kuwapa mashabiki, tunawaomba mashabiki kushiriki kwa  nguvu zote,” alisema Rugambo.
Alisema kuwa wamejipanga kufanya zoezi hilo na lengo kubwa ni kuwazawadia mashabiki wao ambao na kufaidika na tamasha hilo.
Kwa mujibu wa Rugambo, zawadi zote zipo katika mikoa ambayo fiesta imefanyika na ndiyo maana wameweza kutoa zawadi mkoani Kigoma mara baada ya kuchezesha droo.

No comments:

Post a Comment