TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 22 August 2013

TGNP yakutana na wakazi wa Mwananyamala kujadili rasimu ya Katiba

Kenny Ngomuo

Na Mwandishi wetu

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imekutana na wananchi wa Mwananyamala wapato 50 kuchambua rasimu ya katiba.

Mwanaharakati  wa TGNP Kenny Ngomuo ameiambia Blogu ya jamii kuwa lengo la kukutana na wananchi ni kutaka kujenga uelewa wa pamoja wa masuala ya Katiba.

Alisema TGNP imeona iwashirikishe wananchi katika kuchambua mapungufu yaliyopo, kwa lengo la kupata mapendekezo  na maboresha ya katiba rasimu kwa manufaa ya wanawake wote.

“Tumeanza kuchambua rasimu ya katiba na leo tuko Mwananyamala, tunaamini kwamba kwa mawazo ya  pamoja tunaweza tukapata maboresho na mapendekezo yatakayoingizwa kwenye katiba mpya, ili kuwasaidia wanawake kupata haki zao,”alisema Ngomuo.

Alisema TGNP itahakikisha wanawake walioko pembezoni  wanatoa sauti zao kwasababu ndio wazalishaji wakubwa.

“Tutahakikisha wanawake walioko pembezoni wanashiriki kikamilifu kwasababu ndio ambao hukumbwa na mfumo kandamizi, ni wazalishaji lakini hawapati haki ya kumiliki rasilimali ardhi,”alisema.

Alisema katika uchambuzi wao, baadhi ya mambo waliyoyapendekeza kabla ya kutolewa kwenye rasimu ya katiba mpya, baadhi yapo ingawa yana mapungufu machache.

Akatolea mfano haki za wanawake limeingizwa lakini halijawekwa kwenye misingi wa haki za binadamu, hivyo bado wataendelea kulipigia kelele ili hatimaye liingizwe.

Haki za wanawake kumiliki rasilimali ardhi, anadai kuwa halijaingizwa kwenye misingi, kwani nalo linahitaji liingizwe huko, kuwapa nafasi ya haki na ulinzi wa shughuli zao za uzalishaji

No comments:

Post a Comment