TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday 11 September 2013

Sunderland kutangaza utalii wa Tanzania Uingereza

Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson(wa pili kutoka kulia) akiongea na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam  juu ya mazungumzo ya awali ya timu hiyo kuanzisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini.Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto) , Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki(wa pili kutoka kushoto) na Mwakilishi wa timu ya Sunderland hapa nchini Edmund Hazzal(kulia)
 

Mkurugenzi wa Biashara wa Timu ya Sunderland ya nchini Uingereza Gary Hutchinson( kulia) akimkabidhi jezi ya timu yake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Leonard Tadeo(kushoto) leo jijini Dar es salaam mara baada ya mazungumzo ya awali ya kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya kutangaza utalii wa Tanzania nchini Uingereza na vilevile kuendeleza michezo hapa nchini. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Dkt. Alyoce Nzuki. 

No comments:

Post a Comment