TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Wednesday 11 September 2013

Taswa SC, Taswa Queens zatesa bonanza la waandishi Arusha

Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya bonanza la waandishi wa habari lililofanyika kwenye uwanja wa General Tyre, Arusha.
Mwandishi Wetu, Arusha
Timu ya Mpira wa pete (netball) ya wanahabari wa jijini Dar es Salaam,Taswa Queen   juzi ilitwaa ushindi katika bonanza la nane la Waandishi mkoa wa Arusha, baada ya kuichapa timu ya chuo cha uandishi wa habari Arusha Arusha(AJTC) magoli 21-1.
Wakati Taswa Queen walikitwaa ubingwa kaka zao, TASWA SC , walishindwa kunyakuwa kombe, baada ya kutoka suluhu na timu ya AJTC katika mchezo mkali wa fainali, ambao ulisitishwa kutoka na kiza wakati wa mikwaju ya penati timu hizo, zikiwa zimefungana 1-1.
Kutokana na matokeo hayo, Meneja wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL), Endrew Warden alikabidhi Mwenyekiti wa Taswa SC Majuto Omar fedha taslim 200,000 na meneja wa AJTC Modaha Lucas alikabidhiwa kiasi cha sh 200,000.
Taswa  SC, walifanikiwa kuingia fainali baada ya kuichapa timu ya Radio 5 magoli 3-1 na baadaye kuifungua timu ya Arusha 1-0 katika mchezo mkali wa nusu fainali.
 
Kwa Upande wa AJTC, waliingia fainali baada ya kuichapa timu ya  Taswa Arusha, 1-0 na baadaye waliwatoa Sunrise radio kwa penati 11-12 baada ya timu hizo kutoka sale.
 
Katika mchezo wa fainali ya mpira wa pete   uliochezwa uwanja wa general Tyre jijini Arusha, Taswa Queen iliicharaza Taswa Arusha 45-0 katika mchezo wa nusu fainali na kuisambaratisha AJTC ambao walikuwa mabingwa watetezi kwa mabao 53-1 katika mchezo wa fainali.
Kutokana na ushindi huo, Taswa Queen walikabidhiwa kikombe na Meneja mauzo wa kampuni ya Megatrade, Gudluck Kway na fedha taslimu 150,000.
 
Katika soka Taswa Dar pia ilifanikiwa kuingia fainali na timu ya AJTC na licha ya kupigiana mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya kutofungana, mshindi alishindwa kupatikana kutokana na kiza uwanjani.
 
Katika michezo mingine, timu ya ORS kutoka Manyara, ilifungwa  na Sunrise 2-1 na baadaye ORS iliwafungua TBL Arusha goli 1-0 na hivyo kutwaa zawadi ya timu yenye nidhamu.
 
Katika tamasha hilo, katika mchezo wa kuku, wanahabari kutoka Taswa SC, AJTC na Taswa Arusha walitamba na kushinda
 
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindi huo huku akiwapongeza wadhamini wao, Delina Group of Companies, Said Salim Bakhresa & Co Ltd  (Azam), DRFA na Kassim Dewji.
 
Tamasha hilo la nane la vyombo vya habari mkoa wa Arusha, liliandaliwa na TASWA Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique na kudhaminiwa na TBL,TANAPA, egatrade,AICC,Cocacola, Pepsi na Wazee Klabu.

No comments:

Post a Comment