Baadhi ya wajawazito wakiwa wamepumzika wodini |
BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2014 IPUNGUZE
VIFO VYA WAJAWAZITO
ZAIDI ya Wanawake 8,700 hufariki duni kila mwaka nchini
Tanzania kutokana na matatizo ya ujauzito na hasa wakati wa kujifungua. Takwimu
hizi zinaonesha takribani wanawake 24 hupoteza maisha kila siku huku
ikikadiriwa mmoja kufa kila baada ya saa moja.
Hata
hivyo wataalamu wa afya wanasema moja kati ya sababu zinazochangia vifo
hivi ni kukosekana kwa huduma za dharura
katika Vituo vya Afya wakati wa kujifungua. Hata hivyo Serikali ya Tanzania
mwaka uliopita katika ahadi zake imeahidi kupunguza vifo hivi kwa asilimia 50
ifikapo mwaka 2015.
“Si sahihi mama
mjamzito kufa wakati wa kujifungua au si sahihi mama huyu kupoteza uhai wake
kwa kuugawa kwa kiumbe anachokileta duniani, hii haiwezi kukubalika. Na
inasikitisha zaidi pale maisha ya mama huyu yanapotea hata kwa mambo ambayo
yanaweza kuzuilika,” anasema Rais Kikwete katika hotuba yake mbele ya Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa (U.N)
Ban Ki-moon.
Wewe
pia unaweza kushiriki katika kupigania kutokomeza vifo hivi kwa akina mama
wajawazito pamoja na watoto. Je, unataka kushiriki? Tafadhali fuata kielelezo/link
hii hapa chini:-
No comments:
Post a Comment