KITUO cha maombi ya
Visa cha Canada (CANVAC) kimezindua huduma itakayotumia vifaa vya utambuzi wa
binadamu (Biometrics) ambavyo vitatumika kwa wale wote watakaokuwa wakiomba
visa ya kwenda nchini Canada.
Vifaa hivyo vitatumika
kuchukua alama ya vidole ya mwombaji
pamoja na picha zake ambazo zitasajiliwa na kuhifadhiwa mtandaoni.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyosambazwa kwa vyombo vya habari na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)
na kusainiwa na Ofisa wa CANVAC, Katy Kobelski, nchi za Afghanistan, Jamhuri ya
Kimemokrasia ya Congo, Eritrea, Namibia, Pakistan, Sudan Kusini na Yemen ndio
zitakazoanza kutumia huduma hii.
Taarifa hiyo ilisema
kwamba, kwa raia wa Tanzania hawatalazimika kutumia huduma hiyo wakati watakapokuwa
wanafanya maombi ya Visa za Canada.
Katy alisema kuwa
uanzishwaji wa huduma hiyo hapa nchini utapunguza upotevu wa muda na gharama ya watu
kutakiwa kusafiri kwenda Nairobi kwa ajili ya kuchukuliwa alama za vidole, kwani
sasa huduma hiyo itapatikana katika kituo cha CANVAC cha Dar es Salaam.
Novemba 19 mwaka 2013
IOM kwa kushirikiana na ubalozi wa Canada jijini Nairobi, walizindua huduma
hiyo nchini Kenya.
Katy alisema faida ya
huduma hii ni kwamba inafanyika kwa haraka na itamfanya muoambaji kuweza kupata
taarifa zake kwa njia ya barua pepe.
No comments:
Post a Comment