TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Tuesday 4 February 2014

Mbio za mwisho za Paula Radcliffe

Mwanariadha wa Uingereza Paula Radcliffe analenga kukimbia kwa mara ya mwisho katika mbio za London Marathon za mwaka 2015.

Mwanadada huyo wa miaka 40 aliweka rekodi ya dunia katika mbio za Marathon huko Uingereza mwaka 2003 na ameshinda mbio hizo mara tatu.

Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni Radcliffe alikumbwa na jeraha la mguu lililomsumbua na kumfanya kujiondoa katika michezo ya olimpiki iliyochezwa London 2012.

Licha ya Radcliffe, kushinda taji la dunia la Marathon 2005, hajashiriki katika mbio hizo za London tangu 2011 na hajajihusisha na Marathon tangu amalize wa tatu huko Berlin, Septemba, 2011.

Kwa sasa anafanya mazoezi na timu yake ya Uingereza nchini Kenya.

Radcliffe amewahi kushinda mbio za Marathon za New York na amesema kuwa hatastaafu kabla hajashiriki mbio moja ya Marathon.

Mara Yamauchi ambaye ni mwanamke kutoka Uingereza na ana muda bora zaidi baada ya Radcliffe aliiambia BBC Radio 5 live: "Sidhani kama anaweza kurejelea rekodi ya dunia aliyovunja ya 2:15, lakini nadhani anaweza kufikisha 2:20”

Chanzo.Bbc Swahili

No comments:

Post a Comment