TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday 20 February 2014

Xdent hiyoooo mtaani, kazi ni kwako

MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya usambazaji wa filamu za kiswahili Lufingo Exaud amesema kuwa wameingiza mtaani filamu yao mpya ijulikanayo kwa jina la Xdent ambayo imeshirikisha wasanii mbalimbali wenye majina.

Utakutana na King Majuto, Muhogo Mchungu, Lufingo, Mzee Pembe na wasanii mbalimbali walio bobea katika sanaa hii ya filamu nchini.

Filamu hiyo iliyorekodiwa kwa ubora wa hali ya juu na umakini mkubwa yenye mafundisho ndani yake itakuwa chachu kwa jamii kujirekerbisha ka.

Kwa sasa filamu hiyo inapatikana maduka yote yanayouza kanda za kiswahili nchini na mikoa yote
hivyo wapenzi wa filamu wanahimizwa  kununua dvd halali ili waendelee kukuza kipato cha wasanii.
 
Exaud alisema  filamu hiyo imekuwa ikigombaniwa sokoni kutokana na ubora wake pamoja na wasanii wenyewe jinsi walivyo onesha uwezo mkubwa wa kuitendea haki.

No comments:

Post a Comment