Benki ya CRDB PLC imeshinda tenda ya kutengeneza tiketi za elektroniki za
kuingilia uwanjani iliyotangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Kampuni saba zilijitokeza katika
hatua ya awali ya kuonesha nia (Expression of Interest) kwa ajili ya tenda hiyo
ambapo Aprili 19 mwaka huu Kamati ya Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi
ya Tenda ya shirikisho ilipitia maombi hayo na kupitisha nne kati ya hizo.
Baadaye kampuni hizo nne; CRDB
Bank PLC, Prime Time Promotions, Punchlines (T) Limited na SKIDATA People
Access Inc. zilitakiwa kuwasilisha rasmi tenda zao zikionesha jinsi
zitakavyofanya shughuli hiyo pamoja na gharama ya utengenezaji kwa tiketi moja.
Bodi ya Tenda ya TFF ilikutana
Julai 13 mwaka huu kwa ajili ya kupitia tenda hizo ambapo kampuni zote nne
zilifanya uwasilishaji (presentation) wa jinsi zitakavyofanya shughuli hiyo, na
baadaye kuipa kazi hiyo benki ya CRDB.
Uamuzi huo wa Bodi ya Tenda
uliwasilishwa mbele ya Kamati ya Utendaji ya TFF. Kamati ya Utendaji ya TFF
katika kikao chake kilichofanyika Julai 14 mwaka huu iliridhia uteuzi huo wa
benki ya CRDB.
Baadhi ya vigezo ambavyo Bodi ya
Tenda ya TFF iliangalia na kuipa CRDB tenda ni uwezo wa kufanya kazi hiyo
(capacity), hadhi yake mbele ya jamii (credibility) katika shughuli inazofanya
na teknolojia ya kisasa itakayotumika kutengeneza tiketi hizo.
Uamuzi wa TFF kutangaza tenda
hizo ulilenga kuimarisha udhibiti wa mapato ya milangoni na kurahisisha
mtiririko mzima wa washabiki kupata tiketi na kuingia viwanjani.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga
amesema: “Hatua hii ni muhimu sana, kwani tulikuwa tukiisubiri kwa muda mrefu.
Si tu itaimarisha udhibiti wa mapato, bali pia itaondoa matatizo ya tiketi na
kuendelea kujenga credibility (kuaminika) ya TFF. Mafanikio haya si kwa TFF
pekee bali mpira wa miguu kwa ujumla.”
CRDB imeanza mara moja mchakato
wa shughuli hiyo ambapo tiketi hizo zinatarajia kuanza kutumika rasmi katika
kipindi cha kati ya miezi miwili na mitatu kuanzia sas
No comments:
Post a Comment