Young Killer |
Eriki
Msodoki maarufu kama Young Killer ni msanii mdogo na chipukizi katika tasnia ya
muziki wa bongo. Alizaliwa miaka 19 iliyopita jijini Mwanza katika familia ya
watoto sita, na yeye akiwa ni mtoto wa mwisho.
Ni msanii ambaye ana kipaji kikubwa, jinsi
anavyoimba muziki wa bongo fleva mtaani hupenda kusema muziki wa kufoka foka au
mchano, utafikiri ni msanii ambaye aliwahi kuwepo katika sanaa hiyo kwa muda
mrefu kutokana na kuimba kwa kujiamini akiwa stejini.
Kila
mwanamuziki ukimuuliza ulianzia wapi kuimba muziki, wengine watakwambia shule
na wengine watakwambia wamerithi kipaji pengine kutoka kwa baba, mama, mjomba,
dada, kaka na shangazi.
Kwake yeye
young killer anakwambia alianza kupenda muziki
wakati huo akiwa anasoma darasa la tatu katika shule ya msingi Lake
Mwanza. Anasema alikuwa akipenda kusikiliza na kufuatilia muziki na hata kuimba kipindi anapokuwa amekaa mwenyewe.
Mbali na
kuimba, alikuwa akipenda pia kufuatilia muziki sio tu wa Tanzania hadi wa
kimataifa. Msanii ambaye alimvutia kuingia katika muziki ni msanii wa Marekani
Lil Bow na mwingine wa Tanzania ni Fid Q, kwani anavutiwa sana na jinsi
wanavyochana mistari.
“Wanamuziki
hao nawakubali sana ndio walinifanya leo hii mimi nifanye vizuri, nimekuwa
nikiwafuatilia jinsi wanavyoimba, na mimi nimekuwa nikijitahidi kufuata nyendo
zao ili niweze kufika mbali kimuziki,”anasema.
Historia ya
Lil Bow ya muziki ilikuwa inaonyesha kuwa alianza muziki akiwa na miaka mitatu,
na aliendelea kutamba na kufahamika sehemu mbalimbali duniani, na kupata
mafanikio makubwa.
Hali
kadhalika, Fid Q, ni msanii mkongwe
anayekubalika Tanzania na kimataifa, ambaye ana mafanikio makubwa kimuziki.
Young Killer
anasema yeye pia alianza muziki akiwa ni mtoto, alikuwa anasoma lakini pia
muziki aliupa nafasi yake ingawa
hakupata nafasi ya kurekodi hadi alipomaliza darasa la saba mwaka 2008.
Msanii huyu
anajivunia kuwa licha ya kuwa alikuwa akiimba muziki wakati anasoma lakini aliweza kufaulu kwenda Sekondari ambapo mwaka 2009 alijiunga na shule ya Sekondari ya Mwanza.
“Nilipofanikiwa
kuingia kidato cha kwanza niliendelea na muziki, na hapa niliupa kipaumbele
zaidi, kwani nilikuwa najitahidi kutafuta sehemu za kuimba ili kipaji changu
kionekane,”anasema.
Anasema
alikuwa akichanganya masomo na muziki kwani wakati wa usiku alikuwa akihudhuria
klabu mbalimbali za Mwanza na kuomba kuimba jukwaani.
Hakuona
shida wala madhara ya kuchanganya muziki na masomo, alikuwa ana ratiba zake,
kuna muda wa kusoma na muda mwingine alikuwa akijichanganya klabu.
Anasema
alikuwa akipata changamoto kubwa kutafuta shoo kwani wakati alipokuwa akienda
katika klabu mbalimbali kwa ajili ya kuomba kuimba, alikataliwa kwa vile
alikuwa akionekana bado ni mtoto.
Hata hivyo,
alikuwa sio mtu wa kukata tamaa, baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari,
alikutana na mtayarishaji wa muziki aliyefahamika kama Duke, ambaye walisaini
kufanya kazi pamoja chini ya studio inayoitwa Dar Laboratori.
Chini ya
studio hiyo alifanikiwa kurekodi kwa mara ya kwanza wimbo wake unoitwa Tungo
ambapo aliimba kwa staili ya kufoka foka,lakini haukufanya vizuri na hivyo pia hakusikika sana.
Anasema
akarekodi tena nyimbo zake nyingine kama tunaumia, winner, matatizo na chambua
lakini zote hizo hazikufanikiwa kufanya vizuri.
Msanii huyo
anasema hakukata tamaa aliendelea na juhudi za kupambana ili aweze kutoka na
kufahamika.
Kwa bahati
nzuri, mwaka 2012 kulikuwa na shindano la kusaka vipaji lililokuwa linaitwa
Fiesta super nyota ambalo liliandaliwa na kituo cha utangazaji cha Clouds kwa
mikoa yote Tanzania, lengo likiwa ni kupata vipaji vitakavyowakilisha katika
tamasha la Fiesta.
Anasema
walipofika Mwanza alijitokeza akiwa na vijana wengine wengi ili kupata nafasi
ya kutangaza kipaji chake. Anasema kila mmoja aliimba, nay eye ndiye aliyekuwa mshindi
wa jumla akitokea Mwanza.
“Nilishukuru
kwasababu kipaji changu kilionekana na
hatimaye mimi nilichaguliwa kuwa mshindi kwa upande wa Mwanza,”anasema.
Anasema kwa
mara ya kwanza aliweza kupata nafasi ya kufanya shoo za fiesta Mwanza, na
kufanikiwa kuzunguka mikoa yote ya Tanzania na wasanii wakubwa na kufanya nao
shoo mbalimbali.
Kubwa ambalo
anasema hatosahau katika maisha yake ya kimuziki, mara baada ya kupata nafasi
alipanda jukwaani na kuimba maiki moja
na msanii wa Marekani Riki Rose, kwani hakuwahi kuota kukutana naye wala
kupanda jukwaa moja, hilo kwake lilimpa faraja kubwa.
Anasema ni
jambo hatolisahau akiamini kwamba Tanzania kuna wasanii wengi wakubwa, lakini
hawajawahi kupata nafasi kama hiyo ya kuimba jukwaa moja na msanii huyo, lakini
yeye ni msanii mchanga mwenye bahati kubwa.
Wakati
anatoka katika mzunguko wa fiesta tayari mkataba wake wa mwanzo ulikuwa
unaisha, hivyo akapata tena nafasi ya kujiunga na studio nyingine ambayo yuko
nayo hadi sasa inaitwa Classic Sound chini ya mtayarishaji wa muziki Mona
Gangstar.
Anasema
kupitia mkataba mpya, ndipo alianza kuitambulisha ngoma yake mpya inayoitwa
Dear gambe, ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika chati za muziki wa bongo
kutokana na mashairi yake kuwagusa watu.
“Nashukuru
Mungu wimbo wangu wa dear gambe unazidi kufanya vizuri kwani ndio wimbo ambao
unanifanya nipate shoo, kutokana na kukubalika kwa mashabiki wangu,”anasema.
Mbali na
wimbo huo, siku za karibuni aliachia tena wimbo mwingine unaoitwa jana na leo
aliomshirikisha Stamina na Quick Racka, na bado unaendelea kufanya vizuri.
Na sasa bado
anaendelea kuvuma na ngoma yake inayofahamika kama ‘Mrs superstar’.
Young Killer
ni msanii mdogo lakini ana akili nyingi, anajivunia kwamba baada ya kupata
fedha kutokana na shoo za Fiesta na kupitia muziki wake wa dear Gambe, alinunua
mchanga tela mbili na sementi mifuko mitatu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yao
ya kifamilia.
Anasema kwa
jinsi walivyojipanga katika familia yao, kila mtu alipangiwa anunue kitu chake
ili kukamilisha ujenzi wa nyumba yao, nay eye hivyo, ndio vitu ambavyo
alipangiwa na familia yake.
Pamoja na
hayo, anasema akipata mafanikio makubwa kimuziki atamjengea mama yake nyumba
nzuri, kumpa gari ya kutembelea na kutoa mitaji kwa ndugu zake ambao wanaishi
katika mazingira magumu ili wafanye biashara itakayowakomboa.
napend unacho kifany nataman cku 1 nije kuwa kama wew
ReplyDeleteBig up sana young killer
ReplyDeleteNakubl xana msodoki
ReplyDeletemakini sna killer, salute ma men
ReplyDelete