Tahadhari hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa TAREA Injinia Mathew
Matimbwi baada kupata taarifa ya wananchi wa mikoa ya Kilimanjaro, Manyara
na Arusha kulizwa hasa baada kuuziwa vifaa vinavyojulikana kama solar
panel na baadaye kugundua kuwa havifanyi kazi.
Akizungumza na blogu hii jijini Dar
es Salaam Matimbwi alisema alipata taarifa kutoka kwa msamaria mwema ambaye
alikuwa ni mwakilishi wa wananchi wa kijiji cha Magadini Simanjiro ambaye
alikujana risiti mbili zenye anwani ya Kampunii hiyo akitafuta ilipo kampuni ya Solar Afrique ili waweze
kurudishiwa fedha zao.
Msamaria huyo ambaye ni mwalimu wa
shule ya Msingi Emmanuel Madauda alisema wananchi hao walipouziwa
walielezwa wavichaji vifaa hivyo kwa masaa manane kisha wavitumie lakini
walivyofanya hivyo na kuvijaribisha vikawa havifanyi kazi.
Alisema mfanyabiashara aliyewauzia
alijitambulisha kwa jina moja la Bernad ambapo
alitoa namba zake za simu na akidai kampuni hiyo iko Ubungo Plaza na Mwanza
lakini Mwalimu huyo alipoenda kuitafuta Ubungo Plaza akaelezwa hakuna Ofisi za
kampuni hiyo katika Ofisi za Ubungo Plaza kumbe ilikuwa ni danganya toto.
“Jambo la ajabu mfanyabiashara huyo
akipigiwa simu hapokei inaita tu na kukata na namba za simu za kampuni
zinazoonekana kwenye risiti ambazo amekuwa akizitoa pia hazipokelewi,” alisema
Injinia Matimbwi.
Hata hivyo, baada ya Mwalimu huyo
kufuatilia pale Ubungo Plaza alielezwa hakuna Kampuni kama hiyo na hivyo kupewa
orodha na kampuni zilizoko pale na ndipo kuelekezwa akaulizie TAREA ili
wamsaidie.
Mwalimu huyo alibeba risiti mbili
zenye majina ya wananchi waliouziwa vifaa hivyo feki kama ushahidi ili aje
kuulizia kwenye kampunii hiyo ikiwezekana warudishe fedha zao.
Kwa mujibu wa Mwalimu Madauda
alisema Bernad ambaye ndiye mfanyabiashara huhisiwa kwamba ni raia wa
Kenya kutokana na lafudhi ambayo alikuwa akiongea ila amekuwa akiuza bidhaa
hizo nchini kwa madai kuwa ni za hapa nchini wakati hiyo Kampuni haipo.
Matimbwe alisema mbaya zaidi vifaa
hivyo wananchi wa mikoa hiyo wamekuwa wakiuziwa kwa bei ya shilingi 40,000
wakielezwa ni bei ya promosheni lakini ukweli haviuzwi kwa bei hiyo wala
haviuzwi kimoja kimoja kama ambavyo wananchi wameuziwa.
Alisema kutokana na tukio hilo
wananchi wanatakiwa kujifunza kutokana na makosa na kwamba watazungumza na tume
ya ushindani ili kushughulia tatizo hilo ili ikiwezekana wahusika wachukuliwe
hatua kwa kuuza bidhaa feki.
No comments:
Post a Comment