Kupata
huduma ya Airtel money sasa piga *150*60# Bure
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kuboresha huduma
ya Airtel money kwa kurahisisha upatikanaji wa muongozo (menu) kwa kupiga *150*60#
Bure pamoja na kuzindua promosheni kabambe itakayowawezesha wateja wa
Airtel nchi nzima kutuma pesa Bure
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa
Airtel Jackson Mmbando alisema” Airtel tunaendelea kutoa uhuru kwa wateja
kupata huduma zetu kirahisi zaidi nchini kote, kuanzia sasa mteja akipiga *150*60#
anapelekwa mojakwamoja kwenye horodha yake ya huduma na kuweza kuchagua
anachohitaji kufanya ikiwa ni pamoja na kuongeza salio, kufanya malipo, kutoa
pesa na mengine mengi
Tumefanya hivi hii ili kumwezesha mteja mwenye simu yeyote kupata
huduma za kibenki na kuondoa changamoto zozote zitakazojitokeza, sasa mteja
anauhuru wa kuchagua kutumia njia ya awali ambayo ni kwenda mojakwa moja kwenye
muongozo wa simu yake na kupata horodha(Menu) ya Airtel au kupiga namba *150*60#
na kuunganishwa moja kwa moja
Vilevile tunayofuraha kuzindua ofa kabambe kwa wateja wetu nchini
zima ambapo kutuma au kupokea pesa chini ya kiwango cha 100.000 ni BURE na
mteja atakaponunua LUKU kupitia Airtel money ni BURE (hakuna viwango vya
miamala vitakavyotozwa). Tunawajulisha wateja wetu wote na wakala wetu
waliosambaa nchi zima kutumia huduma hii iliyorahisi ni rahisi aliongeza”
Mmbando
Airtel ni mtandao ulioenea nchini na unatoa huduma za kifedha za
Airtel money yenye mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa maeneo mbalimbali mjini
na vijijini kwa dhamira ya kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma za
kifedha na kusaidia wateja wetu kuokoa muda kwenda mbali kupata huduma za
kibenki.
Kupitia Airtel money mteja anaweza kupata huduma mbalimbali
ikiwemo: kupokea pesa, kulipa bill kama DSTV, LUKU na DAWASCO, USA visa ,
kununua salio na huduma nyingine nyingi
No comments:
Post a Comment