Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mnafu Enterprises imeahidi kutoa zawadi
ya seti moja kwa timu ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo nchini (Taswa
FC) kwa ajili ya matumizi katika michezo yake mbali mbali
Mkurugenzi Mkuu wa Mnafu Enterprises, Mnafu Mmary
alitoa ahadi hiyo juzi mara baada ya mechi ya kirafiki baina ya timu Taswa FC
na Salasala Vision Group (SVG) Veterans
iliyofanyika kwenye uwanja wa Leaders Club.
Mmary ambaye pia ni mwanachama mwanzilishi wa timu
hiyo ya Salasala alisema kuwa amevutiwa na timu hiyo ya Taswa FC kwani
wamedhihirisha kuwa wanaandika kitu ambacho wanakijua.
“Nimefurahi jinsi mlivyocheza na kuibuka na ushindi
wa mabao 3-2, nimehamasika sana kwa mchezo wenu na ninaamini kuwa mtaendelea kufanya
vyema,” alisema Mmary.
Alisema kuwa atakabidhi jezi hizo kabla ya mechi yao
ya marudiano iliyopangwa kufanyika Juni 22 kwenye uwanja wao wa Salasala.
Katika mchezo huo wa kuanzisha ushirikiano, Taswa FC
iliibuka kwa mabao 3-2 yaliyofungwa na Majuto “Ronaldo” Omary alyefungwa mawili
yote kwa njia ya mipira ya faulo ndogo nje ya eneo la hatari na Dennis Bukoli
kwa njia ya penati. Mabao ya SVG yalifungwa na Paul Muache kufuatia pasi safi
ya Peter Marwa na Yahya Mbanka baada ya kazi nzuri ya Charles Mtangi.
No comments:
Post a Comment