Na Mwandishi wa EANA
Kenya imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa pili wa Katibu Mkuu wa Jumuiaya ya
Afrika Mashariki (EAC) kuhusu masuala ya sekta binafsi na vyama vya kiraia
utakaofanyika kati ya Oktoba 14 hadi 16, mjini Nairobi.
Uamuzi huo ni miongoni mwa masuala
yaliyojadiliwa wakati wa mkutano wa siku tatu wa wataalamu juu ya utekelezaji
wa majadiliano ya kiushauri kwa ajili ya sekta binafasi na vyama vya kiraia
pamoja na wadau wengine wenye nia na mtangamano wa EAC, uliofanyika mwishoni
mwa wiki mjini Kampala.
Mkutano huo wa wataalamu pia
umechagua kauli mbiu ya mwaka huu kuwa: ‘EAC tunayoitaka.Kulenga Mafanikio ya
Haraka,’’ kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwa Shirika Huru la Habari la
Afrika Mashariki (EANA).
Mkutano wa kwanza wa aina hiyo
ulifanyika mjini Dar es Salaam, Tanzania kati ya Desemba 11 na 12, 2012.
Mkutano huo unalenga kutoa jukwaa la
majadiliano kati ya Katibu Mkuu wa EAC na sekta binafsi pamoja na vyama vya
kiraia juu ya namna ya kuboresha mchakato wa mtangamano ili kuongeza kasi ya
maendeleo ya kikanda.
Wataalamu pia walijadili juu ya
hadidu za rejea kwa ajili ya Kamati za Kitaifa na Kikanda ikiwa ni pamoja na
kujadili rasimu ya utendaji wa Jukwaa la Katibu Mkuu wa EAC.
''Lengo kuu la Jukwaa hilo ni
kuruhusi wadau mbalimbali waliochaguliwa na EAC kushauriana na kufanyakazi kwa
pamoja kufikia malengo ya Jumuiya na kukuza jumuiya yenye misingi kutoka kwa
wananchi wenyewe,'' alisema Mary Makoffi, Mkurugenzi wa Sekta ya Jamii EAC, kwa
niaba ya Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Sekta ya Jamii, Jesca
Eriyo.
Aliongeza kwamba Kamati za
Majadiliano ya Kikanda kwa ajili ya Mkutwano wa Pili, itakutana mwezi Septemba
kuweka mambo sawa kabla ya mkutano wenyewe mwezi Oktoba, mwaka huu mjini
Naitobi, Kenya.
Mapema katika hotuba yake, Mwenyekiti
wa Mkutano, Ronah Serwadda ambaye ni Kamishna katika Wizara ya Afrika
Mashariki nchini Uganda, alisema kwamba Jukwa la Katibu Mkuu wa EAC, ni muhimu
katika kuimarisha na kupanua mtangamano wa kikanda.
No comments:
Post a Comment