Na Mwandishi Wetu
BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa wa Malawi, Chimwemwe
Chiotcha amewasili nchini na kutamba atamtwanga bondia alisyekuwa na mpinzani
Tanzania, Francis “SMG” Cheka katika pambano lao la uzito wa super-middle
lililopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Chimwemwe ambaye hajawahi kupoteza pambano nchini Malawi
zaidi ya kupigwa kwa pointi na Cheka Desemba 27 mwaka jana, alisema kuwa
amekuja kulipiza kisasi huku akiponda matokeo ya awali kuwa Cheka alibebwa
sana.
Alisema kuwa hajui ni ushindi wa aina gani atakaoupata kwa
bondia huyo, kwani Knock Out (KO) au Technical Knock Out (TKO) utokea
ulingoni tu na wala si ushindi wa kupangilia. “Nimekuja hapa kushinda na wala
si vinginevyo, nakuja Cheka amejiandaa sana, sikuridhika na matokeo ya awali na
ndiyo maana nimeamua kuja kurudiana naye, najua nitaibuka na ushindi,” alisema
Chimwemwe.
Alifafanua kuwa si kweli kuwa kila bondia aliyepigana na
Cheka na kushindwa kuwa hajui ngumi za kulipwa zaidi ya hofu tu kutoka kwa
mabondia hao. Mimi nimedhamilia kufanya kweli na ninajua nitashinda, hii ni
fursa yangu,” alisema Chimwemwe ambaye ni mwanajeshi wa Jeshi la Malawi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Best Man Promotion inayoaandaa
pambano hilo, Zumo Makame alisema kuwa maandalizi ya pambano yamekamilika na
siku hiyo kutakuwa na mapambano makali nay a kusisimua.
Makame aliyataja mapambano hayo kuwa, Deo Njiku atawania
ubingwa wa Taifa wa Shirikisho la Masumbwi la PST dhidi ya Cosmas Cheka, Rashid
“Snake Man” Matumla atazichana na Maneno “Mtambo wa gongo “ Oswald na bondia
mwingine kutoka Malawi, Bright Mdoka atazipiga na Jitu Samia.
Mapambano mwngine kwa mujibu wa Makame ni Nasibu Mkude
atapigana na Juma Kihiyo katika uzito wa super welter bout, Juma Afande v Epson
(featherweight) na Karim Mandonga dhidi
ya Ramadhan Agogo katika uzito wa superwelter.
No comments:
Post a Comment