Na Mwandishi
Wetu
KAMPUNI ya
Push Mobile Media Limited itatoa zawadi za magari aina ya Vitz manne (4) na
pikipiki 12 kwa mashabiki mbali mbali watakaoshinda bahati nasibu maalum ya
tamasha la Serengeti Fiesta linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi mjini Kigoma.
Meneja
Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa zawadi mbali
ya magari na pikipiki, pia watatoa zawadi za fedha taslim (sh 100,000) kwa
mashabiki hao ambao ili kushinda wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba
15678 ili kuweza kushinda gari, pikipiki au fedha taslim na unaweza kushinda
tiketi ya VIP kwa kutuma jina la msanii kwa mfano Diamond na kuacha nafasi na
baadaye kuwema maoni yako kwenda namba hiyo hiyo.
Rodney
alisema kuwa mbali ya kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya ndege kuja
Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la fiesta la mwisho.
Alisema kuwa wameamua kuweza zawadi hizo nono ili kunogesha zaidi tamasha hilo
ambalo kwa kuwanufaisha mashabiki wa
muziki hapa nchini.
Aliongeza
kuwa wamejipanga ili kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo kwani
watatoa pia watazindua huduma mpya ijulikanayo kwa jina la Simu TV ambapo
itamwezesha mashabiki kuona video mbali mbali za muziki na matukio mengine,
kupata nyimbo mbali mbali, kupata taarifa mbali mbali ikiwa pamoja na za
michezo kwa kupitia simu ya mkononi.
kuhusiana na
zawadi za fedha, Rodney alisema kuwa zawadi hiyo itakuwa inatolewa kila siku
kwa mashabiki watakaoshinda bahati nasibu hiyo. Alifafanua kuwa jumla ya sh
milioni 80 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili litakalodumu kwa
kipindi cha miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment