Na Mwandishi wetu
Kampuni
ya Delina Group na Chama Cha soka cha Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
kimeipiga tafu klabu waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa SC)
kiasi cha sh milioni 4.2 ili kuwawezesha kushiriki katika mashindano ya
wana-habari yaliyopangwa kufanyika Jumapili ijayo mkoani Arusha.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana kwenye mgahawa maarufu wa City Sports and Lounge uliopo
katikati ya jiji la Dar es Salaam. Katika makabidhiano hayo, mjumbe wa
DRFA kupitia vilabu katika mkutano mkuu wa TFF, Benny Kisaka alikabidhi
kiasi cha sh 1.2 huku Mkurugenzi wa kampuni ya
Delina ambaye ni mdau mkubwa wa michezo nchini, Davis Mosha alikabidhi
shs milioni 3 kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto “Ronaldo De Lima”
Omary.
Kisaka
alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo kutokana na mchango wa waandishi
wa habari za michezo nchini kwa mkoa wa Dar es salaam kwani ni wadau
wao wakubwa.
“Waandishi
wa habari za Michezo wametoa mchango mkubwa wa maendeleo ya michezo
nchini, sit u kwa DRFA, bali kwa vyama vyote vya michezo, sisi DRFA tumekuwa wa kwanza kuonyesha mfano mfano na tunaamini wengine watatuunga mkono ili kufanikisha jambo hili,” alisema Kisaka.
Mosha alisema kuwa amesukumwa sana na mwamko wa waandishi wa habari ambao wameamua kuonyesha kwa mfano kwa kucheza soka na mpira wa pete (netiboli).
Alisema
kuwa kampuni ya Delina Group imeamua kutoa mchango huo ili kuwawezesha
kufanya vizuri katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na kampuni ya Ms
Unique kwa kushirikiana na Taswa Arusha na kudhaminiwa na TBL, Tanapa,
Mega Trade, Pepsi, AICC na Wazee Klabu.
“Huu
ni mchango wangu nikiwa kama mdau mkubwa wa michezo, nimefarijika sana
na tunaamini kuwa mtafanya vizuri katika mashindano hayo ambapo
nimeambiwa Taswa SC ni mabingwa mara mbili mfululizo,” alisema Mosha.
Mwenyekiti
wa Taswa SC, Majuto Omary aliwapongeza wadau hao kwa msaada huo mkubwa.
“Mbali ya DRFA na Davis Mosha, pia Azam imetupiga tafu safari hii
ambapo mbali ya fedha pia wametoa jezi mbili,” alisema Majuto.
Aliwataja
wadhamini wengine kuwa ni Bodi ya Ligi (TPL Board) na Kassim Dewji
ambao wamechangia kufanikisha ziara hiyo. “Bado tunahitaji msaada wa hali na mali ili kuweza kufikia bajeti yetu, kwa ajili ya safari hiyo,” alisema Majuto.
Mwisho…
No comments:
Post a Comment