Lulu wa kwanza (kushoto)Mratibu wa DFF (katikati) Staford Kihore na kulia ni Godfrey Katula ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya Haak Neel Production |
FILAMU mpya
ya Foolish Age ya msanii Elizabeth Michael maarufu kama Lulu inatarajiwa kuonyeshwa
kwenye tamasha la filamu linalofahamika kama ‘Dar Filamu festival’ (DFF)
litakalofanyika Septemba 24 hadi 26 jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa
tamasha la DFF 2013 Staford Kihore amewaeleza waandishi wa habari jana kuwa,
tamasha hilo limeandaliwa na Kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana
na mtandao wa habari za filamu.
Alisema
kupitia tamasha hilo, filamu hiyo na nyingine za kibongo ambazo zinatambuliwa
na Bodi ya filamu Tanzania zitaonyeshwa bure kwenye viwanja vya Posta.
Alsiema
tamasha hilo limelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona filamu za
kitanzania, na zile zinazotumia lugha ya kiswahli pekee ili kutoa fursa kwa
ajili ya vijana na jamii husika kwa ujumla.
“Filamu
zitakazoonyeshwa ni zile zinazotengenezwa hapa nchini katika kutangaza lugha
yetu nzuri ya Kiswahili kupitia kazi zao ikiwa kampeni ya filamu central
kuitangaza lugha hiyo na kuwa ni bidhaa muhimu ulimwenguni,”alisema.
Sanjari na
uonyeshaji wa filamu hizo, pia kutakuwa na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya sanaa ambapo watafundisha masomo ya
uandishi wa muswada, uigizaji na uongozaji wa filamu ambapo makampuni ya
utengenezaji filamu yatatumia fursa hizo kutangaza kazi zao.
Alisema siku
ya mwisho kutakuwa na jukwaa la majadiliano kwa wadau wakiwemo Mamlaka ya
Mapato Tanzania(TRA), wadau wa bodi ya filamu na makampuni mbalimbali.
Naye msanii
wa filamu za kibongo Elizabeth Michael amehimiza watu kujitokeza kwa wingi
kwenye tamasha hilo ili kuwaunga mkono.
Alisema ni
muhimu watanzania wakajenga mazoea kupenda filamu zinazotengezwa nyumbani,
hivyo kufika kwao kwenye tamasha hilo, kutawezesha kuinua kazi zao.
No comments:
Post a Comment