TANGAZA NASI LEO 0712709630,0756631636 BARUA PEPE gmkojera@gmail.com

Thursday, 12 September 2013

Maycan5 kuachia La Aziz Lola kideoni


Maycan5

 MSANII wa kizazi kipya, Masoud Kaftany maarufu kama 'Maycan5,' amesema anatarajia kuachia video ya wimbo wake wa ‘La aziz Lola’ kabla ya kumalizika kwa wiki ijayo.

Alisema wimbo huo wenye maneno mazuri ya kimapenzi umekuwa ukifanya vizuri kwa upande wa redio na anategemea kutengeneza video nzuri itakayowavutia mashabiki wengi.

Alisema toka ameutoa wimbo huo tayari amepata mwitikio wa watu wanaoupenda hasa mikoani na katika ukanda wa Afrika Mashariki, wengi wamekuwa wakimpigia simu na kumpongeza.

“Nafurahi kuona mwitikio wa watu wakikubali wimbo wangu, inaonyesha ni jinsi gani unafanya vizuri, unakubalika, nawahimiza wasubiri na video nategemea kuachia wiki ijayo,”alisema.

Maycan5 alisema wimbo huo tayari umeingizwa katika albamu yenye mkusanyiko wa nyimbo mbalimbali za wasanii wa kizazi kipya inayofahamika kama ‘miongoni mwa sifa’  

Amewaomba mashabiki wake kuendelea kumuunga mkono katika video hiyo pindi watakapoiona mtaani.

No comments:

Post a Comment