SERIKALI ina mpango wa kuanzisha benki ya vijana
amabyo itakuwa ikiwapatia mikopo nafuu ili kuwawezesha kujiajiri wenyewe ikiwa ni hatua ya kuongeza uzalishaji na
kukuza uchumi wa nchi.
Kauli hiyo
imetolewa leo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi
wakati wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu na jinsi kwenye
sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu
Nyerere ,jijini Dares Salaam.
Makamu huyo
wa Rais alisema hayo kufutia chapisho
hilo kuonesha kwamba kundi la vijana
wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi miaka 35 kuwa ni watu milioni 15.6 sawa na
asiliamia 34.7 ya watu wote nchini.
“ Idadi hii ya vijana ikitumiwa vizuri itaongeza
uzalishaji na hatimaye kukuza uchumi wa
nchi na kupunguza umasikini ,” alisema Balozi Seif.
Aliongeza
kuwa Serikali na watu wengine wataendelea kuifanya Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, ikiwemo kuhamasisha
vijana kujiunga na vikundi vya uzalishaji mali ni mojawapo ya mikkati ya
kuendeleza vijana.
“ Kwa kuzingatia rasilimali zilizopo Serikali ina
dhamira ya Kuimarisha viwanda na Kilimo Kwanza kama njia nyingine za kuwazesha
vijana kupata ajira na kuongeza kipato. Vijana wa tabia ya kungojea ajira kazi
za maofisi ambazo haziko nyingi, bali wajiunge na kushiriki katika shughuli za
uzalishaji mali ili waweze kujaipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha
yao,” alisisitiza.
Aidha
aliongeza kwamba kupitia chapisho hilo, limeonesha kuwa kundi jingine
la wazee wenye umri wa miaka 60 au zaidi
amabo ni milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 ya watu wwote nchini. Hivyo kulingana
na Sera ya Wazee kundi hilo
linahitaji huduma maalum kama vile, matibabu, malazi na huduma nyingine
muhimu.
“Serikali na
wadau wengine wataendelea kuwapatia wazee hawa huduma muhimu kulingana na hali
ya uchumi wan chi,” alisema.
Balozi Seif
alizita Wizara ,Idara na Taasisi zote za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kuboresha sera zilizopo na kutumia
takwimu hizi katika kupanga mipango ya maendeleo.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) Dk. Albina Chuwa
alisema chapisho hilo linaonesha kuwa
umri unaoanzia miaka 0 hadi 4 kuashiria kuwa kiwango cha uzazi bado ni kikubwa.
Alifafanua
kuwa kwa kumujibu wa Utafiti wa Mama na
Mtoto wa mwaka 2010 kiwango cha uzazi ni wastani wa watoto 5.4 kwa kila mama
mwenye umri wa miaka 15hadi 49, hivyo
uzazi wa mpango utaendelea kusisitizwa.
Naye Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia (UNFPA)Mariam Khan alisema
chapisho hilo litasaidia kujua iddai ya
watu wanaojiandikisha shule, wastaafu, kupanga uzazi wa mpango na mipango mingineyo.
No comments:
Post a Comment