Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga akiwa ameshika jezi ya Mbeya city hivi karibuni baada ya kukabidhiwa jezi mbali kwa ajili ya timu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara |
BODI ya Ligi
kuu Tanzania bara imehimiza wadau mbalimbali wa soka nchini kujitokeza na
kufadhili michuano ya ligi daraja la kwanza.
Michuano ya
ligi daraja la kwanza inaanza rasmi Septemba 14 hadi mwishoni mwa mwezi Oktoba,
mwaka huu katika viwanja mbalimbali huku kukiwa hakuna mfadhili yeyote aliyejitokeza
kwa ajili ya kudhamini mashindano hayo.
Mkurugenzi
wa bodi hiyo, Silas Mwakibinga ameiambia blogu hii kuwa timu nyingi
zinazocheza ligi daraja la kwanza zinatoka kwenye mazingira magumu zikiwa
hazina vifaa vya michezo huku pia kukiwa na gharama kubwa za uendeshaji wa
mashindano .
Alisema
kutokana na timu hizo kutokuwa na udhamini Bodi ndio hugharamika kununua vifaa
vya michezo kama mipira, bendera na vingine muhimu.
“Tunawahimiza
wadau mbalimbali kujitokeza na kudhamini mashindano ya ligi daraja la kwanza,
zinahitaji kupata udhamini ili ziweze kutoka kwenye mazingira magumu,”alisema.
Alisema kwa
sasa wako kwenye mazungumzo na Kampuni ya EAG kwa ajili ya kuwatafutia udhamini
wa ligi hiyo.
Kwa mujibu
wa Mwakibinga, lengo la kutafuta wadhamini ni kuhakikisha sio tu ligi hiyo inapewa
vifaa bali pia zinapata nafasi ya kutangazwa ili kuweza kuwavutia wawekezaji
watakaojitokeza kuwekeza kwenye soka la Tanzania.
“Nategemea
msimu ujao ligi zetu za daraja la kwanza nazo zitanufaika kama mikakati yetu ya
kupata wadhamini itafanikiwa,”alisema.
Halikadhalika,
tayari ameshaanza mazungumzo na kampuni moja ya utangazaji nchini kwa ajili ya
kununua haki za matangazo ili kurusha ligi daraja la kwanza, na dili
litakapofanikiwa ataeleza ni akina nani.
No comments:
Post a Comment