Na gazeti la Mwanachi
Dar es Salaam. Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi.
Dar es Salaam. Ripoti mpya ya utafiti imebainisha kuwa mishahara mikubwa wanayolipwa viongozi wa juu serikalini na wanasiasa hailingani na utendaji wao wa kazi.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa jana jijini Dar es
Salaam, imeeleza kuwa viongozi hao wanalipwa mishahara inayotofautiana
kwa kiwango kikubwa na pato la mwananchi wa kawaida.
Huku ikitaja mapato ya mishahara ya marais wa
baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania, imesema kuwa hali
hiyo ni kuibebesha jamii mzigo wa kugharimia malipo ya viongozi.
Akizindua ripoti hiyo iliyochunguza gharama za
kuwalipa viongozi wa Serikali na wanasiasa, Mtafiti kutoka Taasisi ya
Utafiti kuhusu Kuondoa Umaskini (Repoa), Dk Theodore Valentine, alisema
kuwa viongozi wa Afrika Mashariki ndio wanaoongoza kwa kulipwa mishahara
mikubwa zaidi chini ya Jangwa la Sahara.
“Kama viongozi wakuu watakuwa wanalipwa mishahara
mikubwa, nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara zitaweza kugharimia
demokrasia?” alihoji Valentine.
Utafiti huo uliofanyika kati ya mwaka 2009 na
2012, umebainisha kuwa Rais wa Tanzania analipwa mshahara dola 172,014
kwa mwaka (Sh275 milioni) sawa na Sh22.9 milioni kwa mwezi, huku Rais wa
Kenya, akiongoza kwa kulipwa dola 515,021 kwa mwaka (Sh824 milioni) kwa
mwaka sawa na Sh68.6 milioni kwa mwezi.
Rais wa Rwanda analipwa dola 199,000 kwa mwaka
(Sh124 milioni) sawa na Sh10 milioni kwa mwezi, wakati rais wa Nigeria
akipokea dola 161,902 (Sh259 milioni) ambazo ni sawa na Sh21 milioni kwa
mwezi.
Pia umeeleza kuwa Rais wa Kenya analipwa mara 320
zaidi ya pato la mwananchi wa kawaida wa nchi hiyo, wakati rais wa
Afrika Kusini anapata mara 46 na Rwanda mara 150 zaidi ya mwananchi wa
kawaida.
Ripoti hiyo imeendelea kubainisha kuwa rais wa
Tanzania analipwa mara 8.2 ya mshahara wa hakimu, huku rais wa Kenya
akipokea mara 13.1 na kumpita rais wa Rwanda anayechukua mara 12 zaidi
ya mshahara wa hakimu.
Kwa upande wa wabunge, utafiti huo umeeleza kuwa
wabunge wa Tanzania wanalipwa mara 3.0 ya mshahara anaolipwa hakimu,
Kenya (5.5) na Rwanda (3.0). Viwango hivyo vimetajwa kuwa vikubwa kuliko
vya wabunge wa Nigeria na Afrika Kusini.
Naibu Spika anena
Naye Naibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job
Ndugai alisema kuwa umefika wakati ambapo mishahara ya viongozi wa umma
inabidi iwekwe wazi kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment