Na Mwandishi Wetu
Miss Universe
Tanzania, Betty Boniface Omara amerejea nchini kutoka Urusi alipokwenda
kushiriki katika mashindano ya kimataifa na kukiri kuwa mashindano hayo ni
magumu pamoja na kupata uzoefu mkubwa.
Betty ambaye aling’ara
katika vazi la Taifa kwa kuvaa vazi lilobuniwa na mbunifu chipukizi, Mwanakombo
Salim kwa kusaidiana na wasanii wa Tingatinga, alisema kuwa pamoja na
kutofanikiwa kuingia hatua ya 16 bora, anachojivunia ni kuweza kuitangaza nchi
kwa kupitia vivutio vya utalii akiw balozi wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA) ambao
walikuwa wadhamini wakuu wa mashindano ya Miss Universe Tanzania.
Alisema kuwa mbali ya hayo, alikuwa mrembo pekee kutoka bara la Afrika aliyechaguliwa miongoni mwa warembo nane kote ulimwenguni kushiriki katika kipindi maarufu mjini Moscow kinachoonyeshwa duniani kote kijulikanacho kama “Let Them Talk” kinachoendeshwa na mtangazaji maarufu Andrey Malakhov.
Alisema kuwa mbali ya hayo, alikuwa mrembo pekee kutoka bara la Afrika aliyechaguliwa miongoni mwa warembo nane kote ulimwenguni kushiriki katika kipindi maarufu mjini Moscow kinachoonyeshwa duniani kote kijulikanacho kama “Let Them Talk” kinachoendeshwa na mtangazaji maarufu Andrey Malakhov.
Betty alisema kuwa katika kipindi hicho ambacho
kinapatikana kwenye mtandao, alionekana kuwafurahisha sana hadhara ya warusi
katika studio na kusifiwa kwa kuwa mrembo wa kipekee na mwonekano wake wa
kiafrika.
Alifafanua kuwa baadhi ya majaji wa mashindano
ya Miss Universe walikuwepo na walieleza kuvutiwa sana na Betty na kumwona kama
mrembo ambaye alikuwa ana nafasi kubwa ya kuingia 16 bora.
“Kipindi chote nilipokuwa Urusi, niliona kukubalika sana na
warusi wenyewe na hata vyombo vya habari vya kimataifa. Nina furaha kubwa sana
kwani kilichonileta nimekifanikisha kwani lengo langu kubwa zaidi ya ushindi
ilikuwa ni kuhakikisha naitangaza vyema Tanzania na vivutio vyake, kama vile
hifadhi za taifa za Ruaha, Udzungwa, Katavi na mengineyo” alisema Betty.
Alisema kuwa kwa msaada mkubwa wa ubalozi wa
Tanzania nchini Urusi, alifanikiwa kufanya mahojiano na gazeti maarufu la
utalii nchini humo lijulikanalo jarida la utalii nchini Urusu linaliitwa “Hot Line travel Magazine.”
Betty alivalishwa na
Mama Schwari, Kiki Zimba (Kiki’s), Kali Elegance na Nasreen Kareem kupitia duka
lake la Anjipai ambapo alimpa nakshi ikiwemo mikufu na hereni mbalimbali katika kukamilishia mavazi yake na
kuonekana kiafrika zaidi.
No comments:
Post a Comment