Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa maoni ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuhusu ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 yatakuwa mchango mkubwa kuhusu nini kifanyike baada ya kumalizika kwa kipindi cha Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG).

Akizungumza
kwa niaba ya viongozi wenzake, Rais Kikwete amesema: “Mada ya mwaka huu ya mkutano
wetu wa CHOGM ya Maendeleo ya Pamoja kupitia Ukuaji wa Pamoja imekuja kwa
wakati unaofaa. Kwa taasisi kama ya kwetu ambayo inawakilisha watu bilioni
mbili kujadili suala hilo hasa kwa kutilia maanani mjadala unaoendelea kuhusu
ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 ni jambo la busara sana.”
Mkutano wa CHOGM ambao ulianza juzi, Ijumaa,
Novemba 15, 2013, umemalizika leo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kumbukumbu ya
Bandaranaike mjini Colombo, Sri Lanka.
Akizungumzia
mkutano huo, Rais Kikwete amesema: “Tunakupongeza Mheshimiwa Rais kwa
maandalizi mazuri ya Mkutano huo. Tunajua siyo kazi rahisi kuandaa Mkutano wa
ukubwa huu. Lakini kwa uongozi wako wa busara na uongozi wako, kwa kusaidiana
na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, kila kitu kimekwenda vizuri.”
Ameongeza Rais
Kikwete: “Kwa niaba ya viongozi wenzangu waliokusanyika hapa jioni ya leo,
napenda kukutakia wewe, Mheshimiwa Rais, kila la heri katika uendeshaji wa
taasisi yetu hii.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
17 Novemba, 2013
No comments:
Post a Comment