THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa
Baba wa Demokrasia ya Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela alikuwa pia kiongozi wa
Tanzania, shujaa wa Watanzania na Baba wa wananchi wa Tanzania kama alivyokuwa kwa
wananchi wa Afrika Kusini.
Aidha,
Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania na Afrika Kusini zina uhusiano wa kindugu na
wa karibu sana kwa sababu ya kazi kubwa iliyofanywa na waanzilishi wa mataifa hayo
mawili, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Mandela.
Rais
Kikwete pia ameelezea historia ya shughuli za ukombozi za Mzee Mandela na jinsi
alivyofika Tanganyika mwanzoni mwa miaka ya 1960, safari ambayo ilifungua msingi
mkuu wa mahusiano kati ya vyama vya siasa za Tanganyika African National Union (TANU) na African National Union (ANC) cha Afrika Kusini.
Rais
Kikwete alikuwa anazungumza katika mazishi ya Mzee Mandela yaliyofanyika leo,
Jumapili, Desemba 15, 2013 kwenye kijiji cha kwao cha Qunu kilichopo kilomita
23 kutoka mji Mkuu wa Jimbo la Eastern Cape wa Mtata.
Rais
Kikwete alikuwa miongoni mwa viongozi wachache walioombwa kuhudhuria hatua hiyo
ya Mzee Mandela ambaye alifariki dunia siku 15 zilizopita nyumbani kwake mjini
Johannesburg, akiwa na umri wa miaka 95.
Katika
hotuba yake yenye nguvu na iliyotoa somo la historia, Rais Kikwete ameelezea jinsi
Mzee Mandela alivyowasili mjini Dar Es Salaam Januari mwaka 1962 akitokea mjini
Mbeya baada ya kuwa amesafiri bila hati yoyote ya kusafiria kutoka Afrika Kusini
kupitia Bechuanaland (Botswana) na Rhodesia Kaskazini (Zambia).
Rais
Kikwete amesema kuwa safari hiyo ililenga kumshawishi Mwalimu Nyerere kuunga mkono
uamuzi wa ANC kubadilisha mwenendo wa mapambano dhidi ya siasa za ubaguzi wa rangi
kwa kutumia silaha badala ya kuwania haki za Waafrika kwa njia za amani kwa sababu
ilikuwa dhahiri kuwa njia hizo zisingeleta matunda yaliyokusudiwa.
Rais
Kikwete amesema kuwa safari hiyo iliyomwezesha Mandela kupata hati ya kusafiria
ya Tanganyika ambayo ilimpeleka Ghana, Nigeria, Ethiopia na Algeria, ndiyo ilifungua
njia ya mabadiliko ya kidemokrasia yaliyokuja kutokea katika Afrika Kusini mwaka
1994, kuleta uhusiano wa karibu sana kati ya nchi hizo na kumfanya Mandela
kiongozi wa Watanzania kama alivyokuwa kiongozi wa Afrika Kusini.
Wageni
waalikwa wameanza kuwasili nyumbani kwa Mzee Mandela kiasi cha saa 10 usiku na shughuli
zenyewe za Mazishi ya Kitaifa ya Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini zimeanza saa
12 asubuhi ndani ya nyumba ya Mzee Mandela kwa wanafamilia kuaga mwili wa marehemu
kwa mara ya mwisho.
Baada
ya kuaga mwili, wanafamilia wameshiriki ibada fupi na kuandaa jeneza kabla ya kuanza
kwa maandamano ya kupeleka mwili wa marehemu kwenye Hema Maalum kwa ajili ya hatua
ya pili ya shughuli za mazishi, hatua iliyohudhuriwa na wageni maalum waalikwa.
Mwili
wa Mzee Mandela ulifikishwa kwenye Hema Maalum kiasi cha saa mbili na dakika 13
asubuhi kwa ajili ya Sherehe ya Kwanza ya Mazishi ya Kitaifa katika historia ya
Afrika Kusini na kuwekwa chini ya jukwaa kuu ambalo lilipambwa na mishumaa 95
iliashiria umri wa Mzee Mandela wakati anaaga dunia wiki mbili zilizopita Desemba
15 nyumbani kwake mjini Johannesburg.
Mazishi
ya leo ambayo yameendeshwa kwa mchanganyiko wa mila na desturi za Kabila la
Xhosa naKanisa la Mesthodist ambalo Mzee Mandela alikuwa muumini wake
yamekamilisha siku 10 za maombolezo ya kiongozi huyo, maarufu kwa jina la Baba
wa Demokrasia ya Afrika Kusini.
Miongoni
mwa watu ambao wamezungumza kwenye shughuli hiyo na kuvutia sana watu alikuwa ni
Mzee Kenneth Kaunda, Rais wa zamani wa Zambia na Mzee Ahmad Kathrada,
mwanasiasa ambaye alifungwa kwenye jela ya Robben pamoja na Mzee Mandela.
Mzee
Kathrada ambaye anasema kuwa alikutana na Mzee Mandela miaka 67 iliyopita,
alifungwa Robben kwa miaka 26 wakati Mzee Mandela alikaa miaka 27.
“Alipofariki
Walter Sisulu nilikuwa nimepoteza baba yangu, sasa kwa kumpoteza Nelson Mandela
nimempoteza kaka yangu. Sina mwingine aliyebakia wa kumkimbilia,” alisema Mzee Kathrada
katika kauli iliyovutia sana hisia za waombolezaji.
Miongoni
mwa wageni hao maalum waalikwa walikuwa ni pamoja na Rais Kikwete na viongozi kutoka
nchi mbalimbali chache wakiwemo wa Malawi, Zambia, Nigeria, Zimbabwe, Lesotho,
Ethiopia na Mama Maria Nyerere.
Kwenye
hatua hii ya pili, wageni maalum wamesikiliza nyimbo za kwaya na hotuba mbalimbali
za viongozi wachache waliopewa heshima maalum ya kuzungumza katika shughuli hiyo
akiwemo Rais Kikwete.
Wengine
waliozungumza ni mwakilishi wa familia ya Mandela Chifu Ngangomhlaba Matanzima,
rafiki wa karibu wa Mzee Mandela Bwana Ahmad Kathrada, Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
(AU) Waziri Mkuu wa Ethiopia Mheshimiwa Hailemariam Daselegn, Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Uchumi ya Kusini mwa Afrika (SADC) Rais Joyce Banda wa Malawi na Rais mwenyeji
Mheshimiwa Jacob Zuma.
Baada
ya hatua hiyo ya pili, mwili wa Mzee Mandela umehamishiwa kwenye kaburi lake ukiwa
unashuhudiwa na waombolezaji maalum ambao ni pamoja na familia yake.
Kwenye
eneo hilo la kaburi, Ofisa wa Jeshi la Afrika Kusini ameondoa medali, bendera na
heshima nyingine ambazo kiongozi huyo amewahi kuzipata katika maisha yake na kuzikabidhi
kwa Mkuu wa Jeshi hilo ambaye naye amezikabidhi kwa Rais Zuma ambaye amezikabidhi
kwa mrithi wa Mzee Mandela.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Desemba, 2013
No comments:
Post a Comment