Jaji katika kesi inayomkabili
Oscar Pistorius anasema kuwa mwanariadha huyo lazima aanza kufanyiwa
uchunguzi wa kiakili kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa mwezi mmoja kubaini
hali ya akili yake alipomuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Amri ya jaji inakuja baada ya shahidi mmoja wa upande wa mashitaka kusema kuwa mwanariadha huyo anakumbwa na matatizo ya kuzongwa na mawazo pamoja na kuwa na wasiwasi wakati wote.
Bwana Pistorius amekanusha madai ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kusudi.
Anasema kwamba kwa bahati mbaya alimpiga risasi kupitia mlango wa choo baada ya kushikwa na wasiwasi akidhani kuwa alikuwa jambazi aliyevamia nyumba yake.
Chanzo.Bbc Swahili
No comments:
Post a Comment