Mwanamuziki wa muziki wa Reggae Innocent Ng'anyagwa akiimba kwenye jukwaa la Sanaa la Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) hivi karibuni. |
Nyota wa muziki wa Reggae Innocent Ng'anyagwa maarufu kama Ras Inno anatarajia kufanya onesho Mbeya Oktoba 10, Songea Oktoba 17 na kwenda kwao Iringa. Pia, atafanya ziara Dar es Salaam, Kahama na Arusha.
Ziara hiyo ni kutangaza albam yake ya Love Story na kusaidia makundi maalum na kuibua vipaji vya wasanii chipukizi wanaopenda muziki huo.
Ras Inno alisema ili kukamilisha ziara hiyo anaomba wadau mbalimbali, Taasisi na Makampuni kumuunga mkono.
No comments:
Post a Comment