Kayumba alishinda shindano hilo juzi ambapo
alijinyakulia kitita cha Milioni 50 pamoja na mkataba wa kusimamiwa kazi zake
za sanaa wa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 10 kutoka Tip Top Connection.
Kayumba alishinda akiwa amemwacha mshindani mwenzake
Nassib Fonabo ambae watu mbalimbali ndio wamekuwa wakilalamika kuwa ndie
alietakiwa kuwa mshindi.
Akizungumzia sakata hilo Jaji Mkuu huyo alisema kuwa
kwa kawaida kazi ya majaji inakuwa ni kuwachuja washiriki kutokea mikoani na
hadi kufikia hatua ya tano bora ambapo kwa mwaka huu ilikuwa ni hatua ya sita
bora kutokana na ushindani kuwa mkali zaidi.
Alisema kuwa ikishafikia hatua hiyo inabakia kuwa ni
kazi ya wananchi kuchagua mshindi na ndicho kilichofanyika siku hiyo na
kujikuta Kayumba akishinda.
Alisema kuwa siku ya mwisho majaji hawana kazi ya
kuwachuja washindi kwa kuwa inakuwa wananchi kupitia kura zao ndio wenye jukumu
hilo.
Aliongeza kuwa Kayumba hadi siku ya mwisho ya kupiga
kura alipigiwa zaidi ya kura elfu 15 na hiyo ilitokana na zaidi uchezaji na
uimbaji wake ambao uliwavuyia zaidi wapenzi wa muziki.
"Sisi kama majaji hatuna ushawishi siku ya
mwisho na hiyo inakuwa ni kazi ya majaji na kwa ushindi huo wa Kayumba ni
wapiga kura wenyewe na sasa sisi tunahusika vipi hapo" alisema Jaji huyo.
Aliongeza kuwa " hakuna uchakachuaji wowote kwa
kuwa washiriki wakibakia wawili kazi inakuwa ni kwa mashabiki katika kuwachagua
washiriki hao wawili na ni wao wenyewe ndio wanakuwa na mbinu za kuwavutia watu
kupiga kura".
No comments:
Post a Comment