Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Taifa Kilimanjaro Stars imetolewa katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati,
CECAFA Challenge baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 dhidi ya wenyeji Ethiopia baada ya kucheza dakika 90 na kupata sare ya bao 1-1.
Katika
mchezo huo wa Robo Fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Kili Stars iliongoza kwa bao lililofungwa na John Raphael Bocco ‘Adebayor’ baada ya kupata pasi ya Deus
Kaseke dakika ya 25.
Ethiopia
walisawazisha kipindi cha pili dk. 57 katika bao lililofungwa na Panom
Gathouch baada ya Mohammed Naser kuangushwa na
Shomary Kapombe
Waliokosa penalti ni Shomary Kapombe na Jonas Mkude huku waliofunga ni Himid Mao,
mshambuliaji Bocco na beki Hassan Kessy.
Waliofunga penalti za Ethiopia ni Panon Gathouch, Mohammed Naser, Ashalew Tamene na Behaylu Girima.
Aidha, Uganda imeifunga 2-0 Malawi mabao ya Farouk
Miya na Ceasar Okhuti na sasa itakutana na Ethiopia katika Nusu Fainali.
No comments:
Post a Comment