Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) Dk. Agnes Kijazi amesema upepo
mkali unaovuma kwa sasa ni upepo wa kawaida ambao unakuwepo kila mwaka miezi
hii na kuwahimiza wananchi kutokuwa na hofu dhidi ya hilo.
Akizungumza na
blogu hii Ofisini kwake jijini Dar es Salaam Dk. Kijazi alisema mabadiliko
yanayotokea hivi sasa ya hali ya hewa yasiwatishe watu.
Pia, alisema
mafuriko yaliyotokea China hayawezi kufika Tanzania, kwa hivyo jamii isiwe na
hofu. Vile vile alisema hiki sio kipindi cha mvua, msimu wake unaojulikana ni
Octoba, Novemba, Decemba na kipindi cha mwezi Marchi, April na Mei.
Kipindi cha
upepo ni Mwezi Juni, Julya na Agost. Pamoja na hayo alisema anatarajia kutoa
taarifa za mabadiliko ya hali ya hewa mapema mwezi Septemba mwaka huu hivyo
wananchi waendelee kufuatilia ili kuchukua tahadhari.
No comments:
Post a Comment