Msanii wa
Muziki wa dansi wa bendi ya Twanga Pepeta Haji Ramadhani ameelezea kwa
masikitiko makubwa jinsi ambavyo baba yake mzazi Mzee Ramadhani alivyofariki
dunia baada ya kupewa sumu.
Akihojiwa katika
kipindi cha Mkasi kinachorushwa na runinga ya EATV, Haji alisema Baba yake alifariki muda mrefu kutokana na kupewa sumu,
kutokana na sababu za kisiasa kwa vile alikuwa ni Mjumbe wa CCM katika ngazi ya
Wilaya.
Alieleza kuwa
hakuna aliyeshuhudia tukio, lakini ushahidi ulijulikana baada ya kufanyiwa
uchunguzi hospitalini na ndipo kubainika alilishwa sumu.
Pamoja na
hayo, haji alieleza jinsi ambavyo mke wake alivyopewa mimba nje ya ndoa na
kudai kuwa ni kitendo ambacho kinamuumiza japokuwa kamwe hawezi kumwacha mke
wake kwasababu anampenda.
Alisema aliogopa
jamii itamuelewaje kwasababu tayari wazazi wa mke wake walifariki dunia na
kumwacha mwanamke huyo mikononi mwake hivyo aliogopa pia kumwacha kwasababu
angepata shida na watoto.
Haji ni baba
wa watoto watatu lakini wawili alieleza kuwa walizaliwa nje ya ndoa kwa maana
kwamba wakati yupo katika mihangaiko ya kutafuta maisha mke wake alibeba mimba
nje kitendo ambacho kilimuumiza.
No comments:
Post a Comment