Na Mohammed
Mhina, wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar
linawashikilia wafanyakazi sita wa meli ya MV Skagit akiwemo mmiliki wake Bw.
Said Abdulrahman pamoja na Nahodha wa meli hiyo Bw. Mussa Makame Mussa na
wanahojiwa kufuatia tukio la ajali ya meli hiyo iliyosababisha vifo vya baadhi
ya abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bandari
ya Zanzibar
Watuhumiwa hao walikuwa wakihojiwa
katika Ofisi za Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mjini Zanzibar ambapo
Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Zanzibar, ACP Yusuph Ilembo, amesema
watuhumiwa hao wawataweza kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Kamanda Ilembo amesema kuwa
Makachero wa Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi na kutafuta taarifa
nyingine zinazohusiana na tukio hilo.
Hata hivyo, Nahodha wa zamu siku ya
tukio hilo la kupinduka na kuzama kwa meli hiyo ya MV Skagit, Bw.Mussa Makame
Mussa, ameelezea kwa ufupi jinsi ajali hiyo ilivyotokea na namna yeye
alivyonusurika katika ajali hiyo.
Amesema kuwa ajali hiyo ilitokea
baada ya kupigwa na dharuba na mawimbi yaliyoambatana na upepo mkali, ambapo
yeye alinusurika kufa maji baada ya kuruka kwa kutumia mlango wa mbele wa meli
hiyo na kuanza kuogelea ambapo alijichanganya pamoja na na abiria wengine
walionusurika na kuokolewa na vyombo vya uokozi.
Wakati huo huo, Wapiga mbizi wa
Vikosi vya Ulinzi na usalama leo wamefanikiwa kuzupata maiti ngingine za watu
watano akiwemo mwanamke mmoja na wanaume wanne.
Katika upekuzi wa maiti hizo,
Makachero wa Polisi walibaini kitambulicho cha kupigia kura kutoka kwa mmoja ya
mwili wa marehemu kitambulicho kilichokuwa na jina la Philip John Busiya
aliyezaliwaq mwaka 1977 katika kijiji cha Mapilinga kilichopo katika Kata ya
Igokelo wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.
Kupatikana kwa miili hiyo mitano,
kunaifanya idadi ya maiti kufikia 73. Maiti nyingine 68 zilipatikana siku za
mwanzo baada ya kutokea kwa ajali hiyo ambapo kati ya hizo, maiti 54
zilitambuliwa na kuchukuliwa na ndugu na jamaa kwa ajili ya mazishi.
Idadi ya miili ya watu waliopoteza
maisha katika boti ya MV Skagit, imeongezeka kutoka 68 na kufikia 73, baada ya
vikosi vya uokozi, kufanikiwa kuopoa miili ya watu watanao, katika eneo la
tukio karibu na kisiwa kidogo cha Chumbe, kilichopo pembezoni mwa mji wa
Zanzibar.
Maiti hiyo iliyopewa namba 72,
pamoja na maiti nyingine nne, zimezikwa katika makaburi ya pamoja ya Kama
yaliyopo nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Eneo hilo la Kama pia lilitumika kwa
kuwazika watu wengine waliokosa ndugu wakati wa ajali ya meli ya Spice Islander
iliyotokea Septemba 9, mwakaja 2911.
Kupatikana kwa miili hiyo,
kumetokana na juhudi zinazoendelea kwa kuvishirikisha vikosi vya ulinzi na
usalama, wazamiaji wa makampuni binafsi pamoja na Mamlaka ya Bandari Zanzibar
wakati wakiwa katika harakati za kuitafuta boti hiyo, ili kuweza kubaini kama
kuna miili mingine iliyosalia kwenye Meli hiyo chini ya Bahari.
Aidha, juhudi za kutaka kuiibua Meli
hiyo zinaendele ambapo wazamiaji wa JWTZ, Polisi, KMKM, JKU, Bandari na wale wa
Makampuni binafsi na wale wa kujitegemea wakiendelea na kazi ya kutafuta mahali
ilipo meli hiyo ili kuona kama wataweza kupata miili mingine iliyonasa kwenye vyumba
vya meli hiyo ambayo imekokotwa na maji kutoka eneo ilipozama meli hiyo.
Source.Swahilivilla
No comments:
Post a Comment