Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini amechaguliwa kuwa Kiongozi wa
kwanza mwanamke wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika AU.
Uteuzi huo umemaliza vutano katika kinyang’anyiro cha uongozi ambao ulikuwa
umetishia kuugawanya na kuudhoofisha Umoja huo.
Kulikuwa na shangwe katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa baada ya
Zuma, ambaye ni mke wa zamani wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kumshinda
kiongozi anayeondoka Jean Ping wa Gabon.
Bibi Dlamini-Zuma aliungwa mkono na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika SADC, naye Ping akipigiwa sauti na nchi za bara Afrika
zinazotumia lugha ya Kifaransa.
SOURCE. Mo Blog
No comments:
Post a Comment