Na Khadija Khamis-Maelezo
Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar imeandaa mikakati ya kudhibiti dawa za kulevya ili kuweza kupambana na
uingizwaji na utumiaji wa dawa hizo nchini .
Akijibu suala la Mhe
Ismail Jussa ladhu jimbo la mji mkongwe alietaka kujua hatua gani zinachukuliwa
na Serikali kuweza kudhibiti madawa ya kulevya nchini, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamo wa Kwanza wa Rais ,Fatma Abdulhabib Fereji alisema wizara
yake itahakikisha mikakati hiyo inafanyakazi ili kuona Zanzibar inakuwa salama
na utumiaji wa dawa za kulevya.
Amesema janga la dawa
za kulevya halina mipaka na kuathiri mustakbali wa rasilimali na nguvu kazi ya
taifa, hivyo juhudi zinahitaji kuchukuliwa katika kuzuiya matumizi ili
kuwaepusha vijana kutumbukia katika janga hilo.
Mh. Fatma amesema
katika kipindi cha mwaka 2010 kuanzia novembar hadi disemba ni kesi 67
zilizokamatwa na januari 2011 hadi juni 2011 ni kesi 168 na kuanzia julai 2011
hadi juni 2012 ni kesi 104.
Alieleza kuwa katika
harakati hizi za kupambana na udhibiti wa dawa za kulevya na uhalifu kwa
ujumla umepungua kutokana na kuimarisha ulinzi shirikishi na taasisi
za dola kufanya doria mitaani pamoja na kuandaliwa kikosi maalum
kikosi kazi ambacho hufichua maficho ya watumiaji na wauzaji dawa za kulevya .
Fereji alivitaka
vyombo vya dola vilivyopewa majukumu ya kupambana na tatizo hilo kuengeza kasi
za utendaji kazi zao ili kunusuru vijana wa taifa letu ambao ni wahanga wakubwa
katika janga hili
Waziri huyo alieleza
kwamba kwa kutambua mchango wa taasisi zisizo za kiserikali katika suala zima
la mapambano dhidi ya dawa za kulevya Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais (OMKR )
kupitia tume ya kuratibu na udhibiti wa dawa za kulevya ilizipatia jumla ya
shilling million tisa na laki tisa (9,900,000/-)nyuma tisa za makaazi ya vijana
wanaoacha matumizi ya dawa ya kulevya (sober house)Unguja na Pemba ambazo
zinatumika katika malipo ya kodi za nyumba chakula na vifaa vyengine vidogo
vidogo vya nyumbani .
Aidha alisema kuwa
Ofisi hiyo imeweza kutoa msaada wa vifaa vya Elektronik ikiwemo Televisheni na
Radio kwa Sober house kwa Unguja na Pemba pia imeweza kutoa mafunzo mbali mbali
juu ya uongozi ,utunzaji kumbukumbu na fedha yameweza kutolewa kwa viongozi wa
makaazi hayo kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uwiano mzuri wa kuweza kukabiliana
na vijana ambao wanaoishi huko ili kuweza kutoa huduma zenye kuleta ufanisi
Waziri huyo
alisema kuwa Wizara yake itaendelea kuunga mkono juhudi hizo na kutoa wito kwa
taasisi nyengine mbali mbali na jamii kwa ujumla kuendeleza kutoa msukumo wa
michango yao ya kuweza kuendeleza mbele harakati hizo .
Source.Full
Shangwe Blog
No comments:
Post a Comment