Kushoto ni
Wema Sepetu, Wastara Juma na Angela Karashani ambaye ni muhusika mkuu katika
filamu hiyo.
MSANII Wastara Juma akiwa na jopo la
wasanii la watu maarufu kutoka katika
kada mbalimbali nchini wanatarajia kuzindua filamu yao mpya itakayokwenda kwa
jina la Sayla.
Filamu
hiyo imepangwa kuzinduliwa katika mikoa minne ambayo ni Arusha, Morogoro,
Dodoma na Dar es Salaam.
Aidha
filamu hiyo itazinduliwa Mkoani Dodoma ambako inatarajiwa Wabunge wanaondelea
na bunge la Bajeti nchini watahudhuria.
Wastara
aliwataja baadhi ya wasanii na watu
mashuhuri waliocheza filamu hiyo kuwa ni pamoja na msanii nyota nchini wa kike Wema
Sepetu, huku baadhi ya watu mashuhuri ni pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika
Mashariki Shyrose Bhanji.
Wabunge
wengine ni Ester Bulaya (Viti Maalum CCM), Halima Mdee na Zitto Kabwe
(CHADEMA), watangazaji maarufu ni pamoja na Maimatha Jesse, Ephraim Kibonde na
wengineo wengi.
Katika filamu hiyo Wastara na yeye
amecheza huku mhusika mkuu ni Angela Karashani , filamu hiyo imeandaliwa na
Kampuni ya Dynamic Minds.
Mwisho
Wastara ambaye ni mke wa muigizaji Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amewashkuru
Watanzania kwa msaaada wao wa hali na mali na kuwataka wamuunge mkono
katika ununuzi wa wa filamu hiyo ambayo mapato yake yatakwenda katika
kumsadia Sajuki na familia yake kwa ujumla.
|
|
No comments:
Post a Comment