Tuzo hizo
kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za Vodacom”
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa
tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri
wao.
Tuzo hizo
ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”, zitatolewa
kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao ikiwa ni kwa mala
ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom.
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa Waandishi wa
mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani
ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
Wapo waandishi
wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali kuhusu
biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja, Ni kwa sababu hii ndio
maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko waliochangia
katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
Baadhi ya sifa ambazo zitapewa kipaumbele
katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni ubunifu na utoaji wa taarifa za
kijamii, Kuzingatia ueledi wa uandishi na uhuru wa vyombo vya habari,
mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa, umahiri wa picha na
ushirikishwaji wa vyombo vingingine.
Waandishi wa mitandao ya kijamii wata
shindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha kuongeza ueledi na umahiri
katika kazi zao.
Kampuni ya Vodacom Tanzania pia
itaanzisha mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali, Kwa mujibu wa Meza
fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha kazi katika
mitandao ya kijamii na tovuti.“Huu ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa ambapo
waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza shughuli zao”,
Alisema Meza na kuongeza kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji
waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi
tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”
No comments:
Post a Comment